JESHI la Polisi, Kitengo cha
Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, kwa kushirikiana na watumishi wa Mamlaka ya
Uwanja wa Ndege (TMA), limemkamata Kwaku Safo (41) raia wa Ghana akiwa na dawa za kulevya aina
ya heroin kilo 12.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam, mkuu wa kitengo hicho, Kamishna Msaidizi Mwandamizi
wa Polisi, Godfrey Nzowa, amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa kwenye Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere JKN jana saa 10 alfajiri.
Kamanda Nzowa amesema kuwa
mtuhumiwa alikuwa akitaka kuelekea Ghana kwa kutukia ndege aina ya KQ
akiwa na hati ya kusafiria namba H2289855.
Nzowa amesema walipata
taarifa kutoka kwa wananchi na kuanza kumfuatilia na kumkuta na kilo 12 za
heroin ambazo alikuwa amezihifadhi katika masanduku yake mawili ya kuhifadhia
nguo.
Amesema kwa mwaka huu,
kitengo chake kimefanikiwa kukamata kilo 228 za heroin na kilo 5 za Cocain
tofauti na mwaka jana ambapo kulikuwa na kilo 264 hali ambayo inaonyesha kuwepo
kwa upungufu mkubwa wa uwepo wa dawa hizo.
KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA