19 WAUWAWA SYRIA


WATU zaidi ya 19 wameuawa katika sehemu mbali mbali za Syria siku moja baada ya Umoja wa Mataifa kulipitisha azimio juu ya kuongeza idadi ya waangalizi wake nchi humo. 

Umoja wa Mataifa unapanga kuwapeleka waangalizi 300 kwa muda wa siku 90 kufuatilia mpango wa   kusimamisha mapigano lakini hadi sasa mauaji yanaendelea nchini Syria. 

Pana wasi wasi mkubwa juu ya usalama wa wajumbe hao na kwa mujibu wa azimio husika, wajumbe hao wa ziada watapelekwa, ikiwa Katibu Mkuu Ban Ki-moon atabainisha kuwa ni salama kufanya hivyo.
Lakini wapinzani nchini Syria wanasema waangalizi wasiopungua 3,000 wanahitajika. 
kwa habari zaidi na BOFYA HAPA