WANAJESHI WATAMANI UTAWARA WA KIRAIA BISSAUU


WATAWALA wa kijeshi nchini Guinea Bissau wanashinikizwa kuurejesha utawala wa kiraia baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutishia kuweka vikwazo, ikiwa viongozi wa wanajeshi hao  walioingusha serikali hawatajiuzulu. 

Watawala hao sasa wanaosema kuwa mpango wao wa kuanzisha kipindi cha mpito cha miaka miwili kwa  kuungwa mkono na upinzani ni pendekezo,ni hatua inayoonekana kuwa ni kurudi nyuma baada ya kutishiwa kuwekewa vikwazo na Umoja wa Mataifa na viongozi wa nchi za Afrika magharibi. 

Marais sita kutoka nchi hizo wanatarajiwa kukutana mjini Conakry leo kuujadili mgogoro wa nchini Guinea Bissau ambako wanajeshi walitwaa mamlaka tarehe 12 mwezi uliopita na hivyo kuzuia uchaguzi wa Rais kufanyika.