ZAWADI ZA MEI MOSI ZATAJWA MORO

KATIBU wa chama cha soka wilayani hapa Kafare Maharagande amezitaja baadhi ya zawadi ambazo zitatolewa katika mchuano wa mpira wa miguu yanayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu ya mei mosi cup.
 
Katibu huyo alisema kuwa zawadi hizo zitatolewa kwa mshindi wa kwanza paka wanne ambapo mshindi wa kwanza atapata seti moja ya jezi,mpira mmoja,stocking na steshengadi, mshindi wa pili atapata seti ya jezi na stocking,mshindi wa tatu atapata mipira mitatu na mshindi wanne atapata mipira miwili.
 
AIdha licha kutaja zawadi hizo zinazotarajiwa kutolewa kwa washindi watakaoshinda katika ligi hiyo alisema kuwa paka sasa katika timu ishirini ambazo zimeshajisajili kushiriki ligi hiyo ni timu kumi na mbili tu ndio ambazo zimeshalipia ada ya kushiriki huo ambapo bado timu nane ambazo hazijatoa bado hivyo kutoa wito kwa viongozi hao kwenda kulipia mapema kwani muda wa kufunga usaili unakaribia kuisha.
 
Hata hivyo alisema kuwa paka sasa timu zimejipanga vya kutosha kuweza kukabiliana na michuano hiyo  ambapo wao kama chama cha soka walitarajia kuwa timu therethini ambazo zitashiriki katika michuano hiyo ingawa paka sasa idadi ya timu zilizolipia ada hiyo bado haijafikia kiwango.
 
Alisema timu nyingi zimejiandaa vizuri kuweza kushiriki ligi hiyo na wanafanya mazoezi ya kutosha, na kwamba alitaja kiwanja kitakachotumika katika kuchezea ligi hiyo kuwa ni uwanja wa The Gunners uliopo sabasaba wilayani hapa.
 
Pia alizitaja timu ambazo zitashiriki katika michuano hiyo ambayo itamalizika kilele cha sikukuu ya wafanyakazi  (MEI MOSI) kuwa ni Mawenzi Maketi,Chamwino Renjaz,Chamwino United,Jamaica Fc,Temino Renjaz,Blak Viba na Moro kids.