CHUNYA INA KABILIWA NA TATIZO LA OFISI ZA MAHAKAMA


KUTOKANA  na kukosekana kwa Gereza la kuhifadhia wafungwa katika wilaya ya Chunya mkoani Mbeya kumepelekea Gereza la Ruanda Mbeya kuto wasimamisha watuhumiwa mahakamani baada ya kukosa mafuta ya gari kwaajili ya kwenda kuwachukua wafungwa hao.

Hayo yalisemwa na hakimu Mfawidhi wa wilaya ya Chunya Ostini Ngatunga wakati akizungumza na ELIABU MTAANI ofisini kwake hivi karibuni.

Ngatunga alisema kukosekana kwa gereza la kuhifadhia wafungwa kumesababisha kuwepo kwa msongamano wa wafungwa katika gereza la Ruanda Mbeya lililopo Mkoani hapa.

Aliwataja baadhi ya watuhumiwa ambao hawajawahi simamishwa mahakamani kuwa ni Daudi Hegela, Rajabu William na Adamu Paul kutokana na kukosa mafuta kwenye gari ya kuwapeleka mahakamani.

Mbali na kukosa gereza gari lililopo lina uwezo wa kubeba wafungwa saba ambapo waliokuwa kesi zao zisisikilizwe na kuahilisha kama watakuwa zaidi ya hapo

Watuhumiwa hao alikuwa wakituhumiwa kwa makosa tofauti tofauti na kuwapo gerezani bila kupelekwa mahakamani kwa muda mrefu.

"Serikali tunaomba ijenge magereza wilayani hapa ili kupunguza msongamano wa wafungwa katika gereza la Ruanda na kucheleweshwa kusikilizwa kwa baadhi ya kesi za wafungwa," alisema Ngatunga.

Aliongeza kuwa kutokana na msongamano huo kunaweza kusabisha magonjwa mbalimbali na kuweza kusababisha serikali iingie gharama za kuwatibu wafungwa.

Vile vile alisema pamoja na kukosekana kwa gereza hilo wilaya hiyo ina ukosefu wa mahakama, kituo cha Polisi ambapo shughuli za kiserikali zina fanyika katika jengo la mkuu wa wilaya ikiwa ni pamoja na mahakama na kituo cha polisi.