TAKUKURU YAWATAKA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO



WANANCHI Mkoani Mbeya wametakiwa kutoa ushirikiano na kutoa taarifa  katika  taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU pale wanapoona dalili za kuwepo kwa vitendo vya kupokea rushwa katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa na mkuu wa taasisi TAKUKURU mkoa  wa Mbeya Bw.Daniel Mtuka,  amesema kuwa wananchi wanatakiwa kutoa taarifa  pale wanapoona rushwa zinatolewa  mitaani na wanaohujumu uchumi nchini.
         
Mtuka amesema kuwa tatizo la rushwa linawezakuzuiliwa endapo wananchi watatoa ushirikiano ili kupambana na tatizo hili sugu nchi Tanzania.

KULIA NI KAMANDA WA TAKUKURU MKOA WA MBEYA DANIEL MTUKA
Mkuu wa TAKUKURU amesema kuwa wananchi mkoani hapa wamekuwa wakijitahidi kutoa taarifa mbalimbali kuhusu watu wanaotoa rushwa, pia amesema mwaka huu jijini hapa wameweza kuwakamata baadhi ya watu wakiwa wanatoa rushwa na baadhi yao kesi zao zipo mahakamani

Pia ameongeza kwa kusema kuwa mwaka huu wamefanikiwa kumkamata wakala wa pembejeo  wilayani KYELA Bw ARPHAN MFILINGE  ambapo alikutwa katika kijiji cha MOGANJI akitoa rushwa kwa wakulima  wa kijiji hicho.

Mtuka ametoa wito kwa wananchi kuwa anawaomba kutoa ushirikiano kwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa kwa kutoa taarifa pale ambapo pataonekana kuna dalili za rushwa kutolewa ili kuwarahisisha raia wao tatizo hilo sugu Tanzania kutokomea