AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUBAKA

JESHI la polisi Mkoani Mbeya linamshikilia mtu mmoja mkazi wa Jakaranda kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wa miaka 10 mkazi wa Mabatini Mbalizi Road baada ya kumdanganya kwa pipi.

Akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya Adivocate Nyombi alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Joseph Kafyoga (17) mkazi wa Jakaranda jijini Mbeya.


Kamanda Nyombi  amesema tukio hilo limetokea march 5 majira ya saa 12;00 jioni katika eneo la jakalanda katika nyumba ambayo mtuhumiwa alikuwa akifanya kazi ya ulinzi ameongeza kuwa mbinu aliyotumia mtuhumiwa ni kumwita mtoto na kudai kuwa alitaka kumpa zawadi ya pipi nakisha kumlawiti na mtuhumiwa amekamatwa na yupo mahabusu .

Wakati huo huo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Waisoni Swila (70) mkazi wa kijiji cha Londoni wilaya ya Mbozi Mkoa ni hapa ameuawa kwa kuchinjwa koromeo na watu wasiofahamika na mwili wke kutupwa katikati ya  barabara ya Vwawa iendayo katika kijiji cha Iganduka.

Kamanda Nyombi amesema kuwa tukio hilo limetokea Machi 5 majira ya saa 2:00 asubuhi wakati marehemu akiwa ametokea katika kilabu cha londoni kijijini hapo na mbinu iliyotumika ni kumvizia marehemu na kisha kumfanyia kitendo hicho.

Aidha ameongeza kuwa chanzo cha mauaji hayo ni imani za kishirikina  kwani marehemu alikuwa anatuhumiwa kuwa ni mchawi  kijijini hapo, hata hivyo polisi wanaendelea na upelelezi ili kuweza kubaini wahusika wa tukio hilo.