LUPA SHWALI SASA




Hali ya ya amani imerejea katika Kijiji cha Lupa Tingatinga wilaya ya Chunya mkoani Mbeya baada ya Serikali, Jeshi la Polisi na familia ya mwanafunzi Saidi Msabaha aliyeuawa na Polisi akidhaniwa mwizi kukubaliana ikiwa ni pamoja na Askari waliosababisha kifo hicho kukamatwa.

Mtoto huyo alikuwa mwanafunzi wa Kidato cha pili katika sule ya Sekondari Lupa ambaye amefariki baada ya kupigwa na Polisi sehemu mbalimbali za mwili wake akituhumiwa kuiba simu ya mgambo wa kijiji.

Awali baba mzazi wa mtoto huyo Mzee Msabaha Huseni alisema kuwa hawezi kuafikiana na Serikali endapo askari aliyehusika na mauaji ya mwanae hatochukuliwa hatua za kisheria.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Wiliamu Mbawala amekiri mtoto huyo alifariki dunia kutokana na kupigwa na askari.

Mara baada ya uchunguzi kukamilika Kamanda wa Jeshi la Polisi Advocate Nyombi alitoa usafiri kwa ajili ya kusaidia shughuli za mazishi ya mwanafunzi huyo na mazishi hayo yamefanyika jana majira ya mchana kijijini hapo. 
 
Ezekiel Kamanga