MADEREVA wa magari ya abilia jijini Mbeya wameiomba serikali kuweza kumalizia ukarabati wa stendi ya daladala ya Kabwe upande wa kuingilia ilikuweza kuweka eneo hilo katika hali nzuri.
Akizungumza na ELIABU MTAANI mmoja wa madereva ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa eneo hilo limekuwa ni kelo kwa madereva kwani wamekuwa wakipata shida wakati wa kuingia katika stendi hiyo.
Mbali na hayo ameupongeza uongozi wa halmashauri ya jiji la Mbeya kwa kujitahidi kuzifanyia ukarabadi baadhi ya stendi na kulifanya jiji la Mbeya kuwa katika muonekano Mzuri.