MACHIFU wapatao arobaini wamekutana Uyole ili kujadili kuhusiana na kongamano la kitaifa litakalofanyika mkoani Morogoro linalotarajiwa kuhusisha mikoa 17.
Moja ya mambo yaliyo jadiliwa katika kipindi hicho ni kwamba kila mjumbe aijue mihimili minne ya muugano huo ambayo ni Machifu, Waganga wa tiba asilia, Wachungaji na Mashehe.
Mwenyekiti wa MUJATA mkoa wa Mbeya Bw Shayo Soja amesema kuwa muungano huo kwa sasa unakabiliwa na changamoto nyingi sana ikiwa ni pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali kama vile Wenyeviti wa Vijiji, Madiwani na baadhi ya wakuu wa wilaya kutotambua umuhimu wa muungano huo na kuwa unafadhiliwa na baadhi ya vyama vya siasa.
Mambo kama hayo ndio yanayo fanya muungano huo ushindwe kufikia ufanisi wa malengo waliyojiwekea katika kukabiliana na maudhi yanayotokea hapa nchini.
Sanjali na hilo Bw Soja ametoa shukrani zake kwa mkuu wa wilaya ya Mbeya Bw Evans Balama kwa kuunga mkono kwa hali na mali ili kusaidia MUJATA inasongambele.
kwa upande wa wajumbe walio changia hoja wachungaji ambao waliwakilishwa na mchungaji Aloice wamesema kuwa hakuna njia yoyote inayo weza kukomesha maovu hapa nchini zaidi ya kumcha Mungu na wao wanapingana na usemi kwamba maovuo ya hapa nchini yanatokana na urithi kutoka Nchi za Nje isipokuwa ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka na ulaji Rushwa ni baadhi ya mambo ambayo yanaweza kuwa ni pigo kwa nchi na kuzaa mambo yafuatayo utoaji Mimba matumizi ya madawa ya kulevya mauaji ya watoto wadogo na upigaji nondo hayo yote yana sababishwa na kumuacha Mungu.