BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA LAANI MAPINDUZI YA MALILAA

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limelaani mapinduzi yaliyofanywa nchini Mali na wanajeshi walioasi, wakilalamikia kushindwa kwa serikali kuangamiza uasi unaofanywa Kaskazini mwa nchi hiyo ya Afrika Magharibi. Baraza hilo lenye mataifa 15 wanachama, limewataka wanajeshi hao walioasi kuhakikisha usalama wa Rais Amadou Toumani Toure, na kurudi kambini mwao. Kufikia sasa bado haijulikani kule aliko rais huyo. Baraza hilo la Usalama pia limezitaka pande zote husika kuwa tulivu na likatoa wito wa kurejeshwa mara moja kwa uongozi wa kikatiba na serikali iliyochaguliwa kwa njia ya kidemokrasia. Wanajeshi hao wa Mali walionekana kwenye televisheni ya taifa mapema Jumatano ili kutangaza kuwa wamechukua madaraka.