HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA YAONGOZA KWA MAAMBUKIZI MAPYA KIFUA KIKUU, ILEJE YAWA NA MAMBUKIZO MACHACHE.


JAMII Mkoani Mbeya inatakiwa kuutambua ugonjwa wa kifuakikuu na kujitokeza kwa wingi kuweza kupima afya zao

Akizungumza na Elimtaa ofisini kwake, Mratibu wa Kifua kikuu Mkoa wa Mbeya Bw. CHAEBY KISONDELA amesema kuwa jamii inatakiwa kutambua kuwa ugonjwa wa kifua kikuu upo katika jamii zetu hivyo ni vyema jamiii ilitambue hilo na kujitokeza mapema kupima afya.

Bw. Kisondela amesema kuwa katika Mkoa wa Mbeya Wilaya ya Mbeya mjini inangoza kwa kuwa na maambukizi mengi ya kifua kikuu lakini Wilaya ya Ileje imekuwa na wagonjwa wachache wa kifua kikuu.

Ameongeza kuwa utolewaji wa elimu ya kifua kikuu umekuwa ni mdogo sana ukilinganisha na elimu ya ugonjwa wa UKIMWI kwani ukimwi umekuwa ukipewa kipaumbele kuliko kifua kikuu hivyo jamii ijitokeeze kupima ili kujua afya zao pindi wanapoona dalili za kukohoa kwa wiki mbili mfululizo ili waweze kupewa matibabu mapema.