KESI YA WAWEKEZAJI WA MASHAMBA YA KAPUNGA YASOGEZWA MBELE.




·      WAKATALIWA HATI ZA KUSAFILIA MPAKA WATOE HATI MUHIMU ZA MASHAMBA.

  • MAHAKAMA YAHOFIA KUTOROKA.




Rubani wa kampuni ya kapunga rice ya mbarali
MAHAKAMA ya hakimu mkazi ya mkoa wa Mbeya leo imetoa masharti ya kuwapatia hati za kusafiria washitakiwa wa mashamba ya kapunga raia wa afrika kusini ambao waliomba wapatiwe paspoti zao ili waweze kutoka nje ya nchi kutibiwa.

Akitoa masharti hayo hakimu anayeiendesha kesihiyo hakimu Seif Kulita amesema baada ya kusikiliza pande zote mbili za washitakiwa na  serikali ndio ameamua kutoa kuwa washitakiwa hao ili wapate hatiza kusafiria lazima watoe hati muhimu za mashamba ya kapunga amayo wanayamiliki ndipo watapatiwa.

Amesema mahakama imeamua hivyo ili kuweka huhakika wa kuto toroka kwa watshitakiwa hao ambao ni raia wa Afrika kusini.

Awali ilidaiwa na wakili wa washitakiwa Aley Luchengula alisema mahakama iwapatie washitakiwa hao watatu hati za kusafiria kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na  mmoja wao akatibiwe nchini Afrika kusini.

Ilidaiwa kuwa Mwingine akabadilishe ambaye ni lubani leseni yake ya kuendeshea ndege wakati mwingine akisema anataka akaogeze muda wa kibali chake cha kuishi hapa nchini ambacho kita kwisha muda wake mwezi April.


Kwa upande wake wakili sa serikali Grifini Mwakapeje alikana kutolewa kwa hati hizo akihofia kutoroka kwa washitakitakiwa katika kesi hiyo.

Katika kesi hiyo wawekezaji hao wamefikishwa mahakamani hapo kwa kosa la kumwaga viwatilifu katika mashamba ya wananchi wa  kapunga ambavyo viliwadhuru na kukausha mazao yao.

Mahakama imesema washitakiwa watapatiwa hati zao maka watimize masharti hayo na kesi imeahirishwa hadi Aprili 17 mwaka huu ambapo itatajwa tena mahakamani hapo.  
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx