Basi la Price Muro Baada ya kupata ajali usiku wa kuamkia jana likielekea Tunduma kutokea Dar es salaam.
Likiwa linaonekana baada ya kupinduka
Hivi ndivyo zinavyo onekana Damu na viti kuharibika vibaya baada ya ajali hiyo iliyo tokea jana usiku
Baadhi ya mabaki ya vitu baada ya ajali hiyo jana usiku
Hili Ndilo Gari la mizigo ambalo basi la Price muro lilitaka kulipita, na baadae kushindwa na kupinduka baada ya kukutana na Gari lengine mbele yake
Shimo hili limechimbika wakati wa ajali hiyo ilipo tokea jana usiku
Hapa ndipo Basi la Prince Muro lilipo taka kuingia na kulikwepa gari hili na kupindukia upande wa pili
Muonekano wa gari hili la mizigo ambalo limeharibikia bara barani
Mmoja wa majeruhi ambae alikuwa anatokea Dar es salaam kwenda kuwasalimu ndugu zake Ileje aliye fahamika kwa jina moja tuu la Andendekisye akiwa katika Hospital ya Ifisi Mbeya Muda huu
Baadhi ya Majeruhi walio nusurika katika ajali hiyo wakiwa katika Hospitali ya Ifisi kuelekea katika matibabu na kutazamwa kama wamepata matatizo yoyote.
Hawa ni majeruhi kati ya wale 14
Mganga mkuu wa Hospitali ya Ifisi Dkt. Mbilinyi akiongea na moja ya majeruhi mapema leo.
Majeruhi ambao wamenusurika katika ajali hiyo mbaya wamesema kwamba dereva huyo alikuwa mwendo kasi tangia walipo fika mikumi, Wameendelea kudai kwamba walimpa onyo mala kadhaa lakini hakuweza kuwasikiliza na akaongeza mwendo kasi zaidi mpaka walipo pata ajali hiyo maeneo ya Senjele kuelekea Tunduma.
Habari kamili itakuja mpaka sasa kuna majeruhi 14 na mtu mmoja amefariki Dunia
Habari kamili itakuja mpaka sasa kuna majeruhi 14 na mtu mmoja amefariki Dunia