MTOTO mchanga asiyefahamika umri, amekutwa ametupwa chooni katika eneo la Chaduru katika Manispaa ya Dodoma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Zelothe Stephen alisema kuwa mtoto huyo alikutwa ametupwa Machi 23, mwaka huu, mchana katika eneo la Chaduru Manispaa ya Dodoma.
Alisema kuwa mkulima mmoja ambaye ni mkazi wa Chaduru, Mwanahawa Ally (68) alitoa taarifa Polisi kuwa ndani ya choo chao kunaonekana kitoto kichanga kimekufa na alimtilia mashaka mkwe wake, Mwajuma Mapuga (34), kwa madai kuwa alionekana kipindi cha nyuma akiwa mjamzito.
Kamanda Zelothe alisema kichanga hicho hakijafahamika kama kilitimiza umri wa kuzaliwa au vinginevyo.
Alisema kuwa mama anayetuhumiwa kutupa kichanga hicho, alitoroka na Polisi Mkoa wa Dodoma inaendelea kumtafuta ili kumtia mbaroni na mwili wa kichanga hicho umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa uchunguzi zaidi.