Ibrahim alisema kuwa binamu yake aliwasiliana na kiongozi wa kidini, kwa ahadi ya kupatiwa kazi. “[Binamu yangu] aliniambia kuwa alikuwa na kazi kwa ajili yangu na nisimwangushe,” Ibrahim alisema. “Kiongozi huyo wa kidini aliniambia nitakuwa meneja mradi katika jumuiya isiyokuwa ya kiserikali.”
Hadithi ya Ibrahim inaonesha mtandao tatanishi wa al-Shabaab unafanyakazi katika miji kadhaa.
“Nilitakiwa kwenda Mandera karibu na mpaka wa Kenya na Somalia, ambako nilichukuliwa na watu ambao ningefanyakazi nao Somalia,” alisema, na kuongeza kuwa wiki mbili zilipita kabla ya mtu yeyote kujitokeza. Ibrahi alisema aliahidiwa shilingi za Kenya 30,000 (sawa na dola za Kimarekani 363) kwa ajili ya kazi hiyo, lakina aliambiwa atasindikisa watoto wawili jijini Nairobi kabla ya kuanza kazi mpya nchini Somalia.
Ibrahim alisema alitakiwa kuwasindikiza wale watoto kupitia vituo kadhaa vya ukaguzi huko Mandera kwa sababu walikuwemo nchini visivyo halali, lakini kwa kuwa yeye ni raia wa Kenya, kuna uwezekano kuwa vikosi vya usalama visingemwuliza. “Baadaye niligundua kuwa mama wa watoto hao, ambaye ni mke wa sheikh, alikuwa ametumia njia nyingine kuelekea Nairobi,” alisema.
“Wakati nilipowakabidhi [watoto] kwa sheikh huko Nairobi, alinitaka niwe mujahidina kwa ajili ya al-Shabaab,” alisema.
Wakati Ibrahim alipomwuliza kiongozi huyo wa kidini kuhusu kazi aliyoahidiwa, hakupatiwa jibu la wazi. “Hapo ndipo nilipogundua kuwa kazi katika shirika lisilo la kiserikali ilikuwa ni hila tu”, alisema, na kuongeza kuwa daima hakulipwa pesa yoyote.
“Ninawajua vijana kadhaa ambao walijiunga na wanamgambo kupitia njia hiyo. Wengine waliacha baada ya kugundua kuwa walikuwa wamedanganywa, wakati wengine walifanyakazi ya uaskari baada ya kuambiwa kuwa watakuwa askari wa kulipwa,” Ibrahim alisema.
“Nilimwarifu baba yangu kuhusu kugeuka kwa tukio hilo na alimwita mjomba wangu na sheikh ili kumwuliza kwa nini alihatarisha maisha yangu nchini Somalia na walighumiwa,” aliiambia Sababhi. Ibrahim alisema aliitembeza kopi ya picha ya kiongozi wa kidini katika sehemu za Garissa, na kuwaonya watu kuwa sheikh alikuwa nyuma ya uandikishaji wa vijana kwa ajili ya al-Shabaab.
Ibrahim alitoa taarifa ya tukio hilo kwa Kitengo cha Polisi dhidi ya Ugaidi huko Garissa mwezi wa Januari, mwezi mmoja baada ya jaribio la kuandikishwa, kusafisha wasiwasi wowote kuhusu uhusiano wake na al-Shabaab. Kuanzia hapo, alisema al-Shabaab walimtishia kwa kumripoti kiongozi wa kidini na binamu yake kwa polisi.
(for more )