SHIRIKA la umeme hapa nchini Tanesco mkoa wa Mbeya ina tarajia kufunga Transifoma katikati ya Mwezi huu katika maeneo mbalimbali ya mkoa huu ambayo hayana au kharibika.
Akizungumza na gazeti hili Ofisini kwake meneja wa Tanesco mkoani Mbeya John Bandiye, alisema wameomba kutoka makao makuu ta shirika hilo Transifoma saba za kufunga katika maeneo mbalimbali ikiwemo kata ya Igurusi ambayo baadhi ya maeneo yake yamekosa umeme kwa muda mrefu kwa sasa.
Alisema wameisha tuma maombi katika ofisi zao kuu Dar es salaam na kuwa waliohahidiwa kutumiwa Transifoma hizo katikati ya mwezi huu na kuzifunga sehemu ambako zina hitajika.
Wakazi wa kata ya Igurusi wamekosa nuru ya umeme katika baadhi ya maeneo ya kata hiyo zaidi ya mwezi mmoja hali ambayo mashine zinazo tumia transifoma hizo kusimama kazi kwa muda wote huo.
Transifoma iliyokuwa ikitumiwa na kata hiyo iliondolewa na Tanesco mara baada ya kuharibika badala ya kuitengeneza kitu ambacho kiliwafanya wananchi kuhisi tofauti.
Baadhi ya wananchi walisikika na gazeti hili wakisema Tanesco imekula njama ya kuondoa mashine za kukoboa mpunga katika maeneo hayo ya makazi ya watu na soko.
Kuhusiana na madai hayo ya wananchi, meneja wa kampuni hiyo, Bandiye alisema Tanesco hawahusiani na madai hayo ya kuhamisha transifoma kwani iliondolewa kutokana na kuwa limeharibika kabisa.
Aliongeza kuwa wao hawaangalii mteja mmoja tu na wanaangalia wateja wote wanao wahudumia kwa kuwapatia huduma zilizo sawa na si kama wanavyo dhani wananchi hao.
Alisema wanaupungufu wa zaidi ya transifoma saba katika maeneo mbalimbali ya mkoa huu wa Mbeya na tatizo hilo litaisha hivi karibuni katikati ya mwezi huu.