KIONGOZI WA HAKI ZA BINADAMU KIZIMBANI KWA KUCHANA NGUO ZA POTI


KIONGOZI wa haki za binadamu amefikishwa katika mahakama ya hakimu mfawidhi ya Vwawa kwa makosa mawili tofauti likiwemo la kuchana Nguo za Askali wilaya ya  Mbozi.

Makosa hayo mawili yalifikishwa katika mahakama ya hakimu Mfawidhi  vwawa ya wilayani humo, mbele ya hakimu MS Mushi, alisema katika kosa la kwanza mshitakiwa alimzuia askali kufanya kazi yake.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mshitakiwa Brown Mwambene ambaye ni mwenyekiti wa haki za binadamu hivi karibuni ilimzuia askali kufanya kazi yake ya kumkamata Wile Waya kwa kosa la kuendesha pikipiki bila kuwa na leseni ya udreva Januari 23 mwaka huu.

Mshitakuwa Mwambene alimzuia askali PC mwenye namba E 6707 Mailosi Bigawa (45) wakati akijaribu kumkamata Waya ambaye alifanya kosa la  kuendesha pikipiki bila kibali ambalo ni kinyume cha  sheria ya makosa ya jinai kifuingu 243 (B) sura 16 ya mwaka 2002.

Ilielezwa mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hili mapema saa 8:00 mchana kabla ya kutenda kosa la pili majila ya saa 10:00 jioni la kumchania askali nguo zake za kazi.
Mshitakiwa alitenda kosa la pili katika harakati za askali huyo kumkamata Waya ambapo alichana nguo za askali huyo wa jeshi la Polisi na kusababisha kushindwa kuendelea na kazi.

Hakimu Mushi alisema mshitakiwa kwa kutenda kosa hilo ni kinyume cha sheria ya makosa ya jinai katika kifungu cha 326 kifungu kidogo cha kwanza (1) cha marekebisho ya sheria ya 16 ya mwaka 2002.

Mushi alisema mshitakiwa alizuia kukamatwa  kwa Waya ambaye alikuwa akiendesha Pikipiki yenye namba za usajili namba T 306 ATV aina ya Sanilag.

Mshitakiwa alikana kutenda makosa yote mawili, hivyo kesi yake imeahilishwa hadi Februali 23 mwaka huu ambapo mshitakiwa atasomewa tena makosa hayo.