BAADHI ya madereva wa magari yaingiayo stendi kuu mkoa wa Mbeya wameulalamikia uongozi wa harimashauri ya jiji kuhusiana na ukarabati wa barabara ya stendi kuu hadi Meta kwa kuweka saruji na kokoto ambazo hazidumu.
Wakizungumza na Mwisae blogu kwa nyakati tofauti mwanzoni mwa wiki hili walisema wanaomba halmashauri ya jiji la Mbeya kuachana na ukarabati wa kutumia saruji na changalawe na kupoteza pesa kila mara.
Wamesema kutokana na uharibifu wa barabara hiyo kuu iingiayo katika stendi kuu unawaathiri sana hasa kufanya uharibifu katika magari yao na maranyingine kusababisha ajari katika barabara hiyo kutokana na kukwepa mashimo yaliyopo.
Mmoja wa madereva hao ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alisema wamekuwa wakiwatoza pesa za ushuru na hawajui pesa hizo zina fanya kazi gani katika serikari ya halmashauri ya jiji hilo kwani kila siku wanalazimika kutoa Tsh1,000 wanapotoka.
Alisema kutokana na malipo hayo kwa kila gari linalipa jumla ya Tsh 60,000 kwa mwezi ambapo na njiani nako wana takiwa kuwalipa Trafki kwa kila kituo na kufikia Tsh 120,000 kwa mwezi na hali ya barabara kuwa bado tete.
Alishauri barabara hiyo bora ingefumuliwa na kujazwa kifusi katika eneo hilo sumbufu na baadaye wakipata fedha za kujenga kwa kiwango cha rami waweke rami katika eneo hilo.
Dereva huyo aliongeza kuwa ni bora kama wangewachangisha pesa yoyote ile ili kuchangia ujenzi wa barabara hiyo na ikaboreshwa kuliko kuenderea kuteseka na ubovu wa barabara hiyo kuu.
Nae dereva mwingine aliyehojiwa kuhusu uboreshwaji wa barabara hiyo Emmanuel Sipian, alisema matatizo yanayo tokana na ubovu wa barabara unawasababishia hasara kubwa hasa kwa kukosa abiria waendao Tunduma kutokana na baadhi ya madereva kuchukulia abiria Mwanjelwa baada ya kuchukulia stendi kuu ambako ndiko wanatakiwa kuchukulia abiria.
Sipiani alisema madereva wengine wanafanya hivyo kwa kukwepa mashimo hayo kutoka Meta hadi stendi kuu kitu ambacho ni kinyume na utaratibu ambao unayataka magari yaendayo Tunduma kuto kwenda Mwanjelwa.
Aidha aliongeza kuwa wamekuwa wakisubili abiria kwa muda mrefu kutokana na abiria wengi kupandia Mwanjelwa na hivyo kupoteza muda mrefu wawapo stendi.
Mbali na suala la barabara Sipian alisema serikali inatakiwa kusimamia kazi vizuri katika vituo vya stendi ya Simike Jijini Mbeya na kuamgalia mari yanayo safirishwa kutoka bandarini kwenda nje ya nchi kutokana na magari hayo kuchukua abiria waendao Tunduma.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Stendi kuu ya Mkoani Mbeya Noah Mwakatumbula, alisema wametoa maralamiko hayo katika uongozi wa jiji la Mbeya lakini haya tendewi kazi vilevile alisema wamekuwa wakitoa ushuru wao na kuto ona kazi inayo fanyia kwasababu kwa mabasi makubwa wamekuwa wakitozwa Tsh 2,000 kwa kodi ya kulala na kutoka wakilipa Tsh 2,000.
Alisema pesa ya kulala basi haieleweki ina fanya kazi gani kwani wanatakiwa wao tena watafute walinzi kwa kila kampuni ya basi wanatakiwa kuwa na mlinzi wake kwa usiku wote basi limapolala hapo stendi.
Mwakatumbula alisema kuwa baraba ra hiyo haitamaniki kutokana na ukubwa wa mashimo Ambato yanatisha na hayafai kuwa katika barabara kuu kama hiyo inayopokea wageni mbalimbali kutoka mikoa tofauti.
Juhudi za kumtafuta Mkurugenzi wa jiji la Mbeya ziligonga mwamba baada ya kumpigia simu bila majibu na baada ye kuzimwa kabisa.