UONGOZI wa mkoa wa mbeya unatakiwa kuweka mbele ajenda ya bima ya afya katika kila vikao vyao vya mkoa ili wananchi wahamasike kujiunga.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya halmashauri ya Mbeya Evans Balama wakati akifungua kikao cha siku ya wadau wa mfuko wa bima ya afya wa mkoani Mbeya uliofanyika jijini hapa.
Amesema viongozi wa mkoa wa Mbeya wanatakiwa kuweka ajenda ya mfuko wa bima ya afya katika kila kikao ili wananchi wahamasike kujiunga na mfuko huo.
Amesema kuwa viongozi na wadau wa mfuko huo kijishughulisha kila siku kilia kiongozi kwa na fasi yake pia ameongeza kwa kuwataka watoa huduma kujiheshimu na kutoa huduma bila kuwa na Dhalau kwa wateja wao.