TIMU YATINGWA NA UKATA WA KIFEDHA

TIMU  ya vijana ya Afirican Boys ya Nzovwe Jiji ni Mbeya  imewaomba wafanyabiashara, makampuni na wadau wa soka, kuichangia timu hiyo fedha ilikuiwezesha kushiriki kikamilifu ligi ya daraja la tatu mkoa
itakayo anza hivi karibuni.


Ombi hilo lilitolewa mapema wiki hii na mwenyekiti wa timu hiyo Allan Kambanga  Sanga alipokuwa akizungumza na MWISAE (BLOGU) jijini Mbeya, aliomba wadau na mashabiki wa timu hiyo kuichangia.

Alisema kuwa anawaomba wadau wa soka wenye mapenzi mema  na timu hiyo
wakiwamo wafanyabiashara na makampuni kuichangia timu hiyo ama
kuidhamini, ambayo kwa sasa inakabiliwa na ukata mkubwa wa fedha
kusudi iweze kushiriki katika ligi hiyo.

Sanga alisema timu hiyo ambayo imekuwa ikishiriki katika mashindano
mdalimbali kama vile mashindano ya mbunge wa Mbeya mjini na mengineyo,
ni ya wana-Nzovwe wote hivyo kutoisaidia nisawa na mzazi kumtelekeza
mwanae.

Timu hiyo ni miongoni mwa timu kongwe zinazo shiriki ligi daraja la
tatu jijini Mbeya na ambayo imewahi kutoa baadhi ya wachezaji mahili
walioshiriki ligi kuu ya soka Tanzania Bara, kama vile Mwamba Mkumbwa
aliye zichezea Mtibwa na Kagera sugar .

Sanga aliwataja wachezaji wengine ni Vincent Barnabas aliyewahi
kuichezea klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam na Moro  united,
pamoja na Shaaban Mtupa wa Tanzania Prison ya Mbeya na Sono Kanu wa
AFC ya Arusha.

Mdau mmoja  wa soka aliye jitambulisha kwa jina la Shomari Ally
amesema kuwa suala la wadau wa soka kuichangia timu hiyo ni la msingi,
lenye lengo la kuleta maendeleo katika katika kuinua kiwango cha
mchezo wa soka hapa nchini.