AFANDE AJINYAKULIA UBINGWA WA DARTS



Afisa wa jeshi la polisi Adelaide Chikoma (kushoto) akipongezwa baada  ya  kushinda kombe ya Darts na mkuu wa polisi wilaya ya Mbeya (OCD)
Adelaide akipongezwa na wafanya kazi wenzake baada ya kutwaa ubingwa huo
Adelaide akipokelewa na wanachi na mashabiki wa mchezo wa darts katika kituo kikuu cha mabasi mkoa wa Mbeya

AFISA  wa jeshi la polisi Mkoani Mbeya Adelaide Chikoma amjinyakuliaubingwa wa vishale Taifa baada ya kumsambaratisha mpinzani wake Paul
Mapunda kwa seti 5-1, katika mchezo mkali wa fainali uliochezwa katika
viwanja vya Rose Garden vilivyopo maeneo ya Area “C” mjini Dodoma hivi
karibuni.


Kwa  ushindi huo Chikoma amejiwekea kibindoni kiasi cha Tsh 150,000
fedha taslim pamoja na kikombe, wakati mpinzani wake Paul Mapunda
amejinyakulia kikombe kidogo na tsh 100,000 kama kifuta jasho.
Mchezo huo uliokuwa wakumbukumbu ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania
(Tanganyika),ulikuwa na upinzani mkubwa, Kwa sababu uliwajumuisha
mabingwa  mbalimbali wa vikombe vya kitaifa hapa nchini.

Alisema kuwa jumla ya washiriki zaidi ya 80 kutoka katika mikoa nane
hapa Nchini walishiriki mashindano hayo ambayo yaliendeshwa kwa mfumo
wa mtoano (Knock-Out).

Chikoma aliitaja mikoa iliyoshiriki katika mashindano hayo kuwa ni
minane ambayo ni pamoja na Dar es salaam, Morogoro, Mbeya, Dodoma,
Mwanza, Kagera, Arusha  na Kilimanjaro.

Alisema kuwa alianza mashindano hayo kwa kupambana na mwenyekiti wa
chama cha Darts Taifa (TADA)  Gesase Waigama Kutoka Dar es salaam,
ambaye alimshinda kwa kumchapa seti 3-0 katika mchezo uliokuwa wa vuta
nikuvute.

Afande huyo aliitaja michezo mingine iliyokuwa na upinzani mkali kuwa
ni kati yake na katibu wa Tada Taifa Mohamed Bitegeko aliye mshinda
kwa seti 3-2, na ule kati yake na bingwa wa zamani wa Taifa Dkt. Mwiru
wa Dodoma ambaye alimchakaza kwa seti 4-0 katika mchezo wa nusu
fainali.

Mchezaji huyo amewahi pia kushiriki katika mashindano ya Polisi ya
kimataifa kwa Nchi za SADC ambazo ni Malawi, Tanzania, Botswana,
Msumbiji, Afrika ya kusini na Zambia, ambayo yalifanyika nchini
Zimbabwe mwaka 2007 na kupata medali ya shaba.

Mwaka 2009 mchezaji huyo alishiriki tena katika mashindano kama hayo
yaliyo fanyika nchini Malawi na kujipatia medali ya fedha na pia
alichaguliwa kuwa mchezaji bora kwa kupiga alama nyingi kuliko
wachezaji wote.


Chikoma alisema kuwa ushindi alioupata huko Dodoma ni wana Mbeya wote
ambao walionyesha ushirikiano mkubwa kwake, kabla ya kufanyika  kwa
mashindano hayo na kumuwezesha kutwaa ubingwa wa Taifa.

Nacho  chama cha vishale Mkoani Mbeya kilimuandalia mchezaji huyo
mapokezi makubwa yaliyo anzia stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani,
na kuzunguka mji wote wa Mbeya hadi kwenye  klabu yake ya Polisi
Mbeya.

Kuhusu matarajio ya baadaye alisema kuwa Mkoa wa Mbeya umejipanga
kufanya maandalizi ya kitaifa, yatakayo fanyika baadaye mwakahuu
ambapo lazima watashiriki.

Kutokana ushindi wake mkubwa alioupata huko Dodoma kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi, pamoja na viongozi wengine wa jeshi
hilo mjini Mbeya walimpogeza nchezaji huyo kwa kuuletea heshima mkoa
na Jeshi kwa ujumla.