AMOS CHUMA AKIWA KATIKA UWANJA WA MPIRA WA TAIFA JIJINI MBEYA NA MWANAE |
KOCHA GWIVAHA WA KWANZA |
Akizungunza na Championi mwanzoni mwa juma hili jijini Mbeya Chuma, alisema ataanzisha mazoezi kwa vijana wa miaka 14 hadi 20 hapa mjini
na huko mawilayani.
Chuma alisema vijana hao watakusanywa kutoka mashuleni na mazoezi yatakuwa yakifanyika sikuza jumamosi na jumapili.
Alisema mazoezi hayo yatakuwa yakifanyikia katika kiwanja cha
kumbukumbu ya Sokoine cha jijini Mbeya na kuazia majira ya saa za asubuhi mpaha mchana.
Chuma alisema kuwa katika mchakato wa kuelekea mawilayani atakuwa akifundisha soka kwa kushilikiana na walimu walioko mawilayani.
Aliongeza kuwa kwa kufanya hivyo kutaongeza taaluma ya ufundishaji wa kwa wale wasio na taaluna na walu wenye taaluma ya ufundishaji wa soka kwa vijana, ilikuwapa misingi mizuri katika mchezo wa soka hata huko
mawilayani.
Kutokana na programu hiyo itasaidia vijana kuwa na uwezo mzuri kisoka na mbinu mbalimbali za usakataji wa kandanda kuanzia huko vijijini wakiwa wadogo na kuwa wazoefu katika mchezo huo wa soka na kuongeza kuwa, Taifa litapata vijana chipukizi katika taaluma hiyo.
Chuma ambaye pia katika miaka ya hivi karibuni amekuwa akiifundisha timu ya mkoa wa Mbeya katika mashindano ya Copa-cocacola alisema kuwa, katika kipindi cha ufundishaji wake amegundua kuwa vijana wengi kutoka mawilayani wanakuwa hawajapata mafunzo ya uchezaji wa mpira kwa sababu ya kukosa waalimu wenye taaluma ya soka kwa vijana.
Alisema kuwa mara baada ya kuandaa mafunzo hayo ataomba apatiwe kibali kutoka chama cha soka cha mkoa wa Mbeya (Mrefa), ili kuweza kutekeleza mpango huo , maana bila wao mpango huo utakwama.
Awali kocha huyo aliifundisha timu ya mpira ambayo ilitamba sana
kipindi cha nyuma mkoani Mbeya ya Tukuyu Star (Banyambala) kuanzia mwaka 2002-2004 akiwa msaidisi wa kocha Paul Gwivaha na pia yeye ni mzoefu katika ufundishaji wa soka la vijana.
Baadhi ya vipaji vilivyoibuluwa na Chuma ni pamoja na aliye kuwa
mshambuliaji hatari wa Tukuyu star na baadaye timu ya Tanzania
Prisons ya Mbeya John Joseph, na Mlinzi maarufu wa kati wa timu
za Tukuyu star na Prisons pia zote za Mbeya Mbega Daffa.
Wengine ni aliye kuwa kipa wa Tukuyu star na Polisi Moro
Emmanuel Mwansile, Mlinzi wa kati Bonifasi Amulike ambaye pia
alizichezea timu za Tukuyu star na Polisi Moro, ambazo zilikuwa
zikishiriki ligi kuu ya Vodacom ya Tanzania Bara wa kati huo.
Orodha hiyo ya wachezaji hao pia inamjumuisha mchezaji
mkongwe Geofrey Bonny ambaye amewahi kuzichezea timu za
Tukuyu star,
Prisons, Yanga pamoja na timu ta Taifa, Taifa Stars, na chipukizi
Omega Semewa Yanga ambaye aliibuliwa katika mashindano ya
kwanza ya kombe la Copa-cocacola yaliyoanza mwaka 2007 hapa
nchini.
Kocha huyo amewashauri TFF taifa wajaribu kuwa kipaumbele
makocha wote wanaojishughulisha na soka la vijana .
kuwaendeleza kitaaluma kuwa kuwapatia mafunzo ya mara kwa
mara ili kwenda na wakati katika mchezo huo unao badilika kila
wakati.
Amewataka pia TFF kuacha mara moja mtindo wanao tumia wa
kuwang’ang’a nia tu makocha wa timu za ligi kuu, bali pia
waelekeze nguvu kwa makocha hawa wanaojitolea kwa kuwa patia
vifaa vya mazoezi, na mafunzo mbalimbali ili kuwatia moyo maana
timu wanazo fundisha hazina wafadhili.