Showing posts with label Tanzania na EAC. Show all posts
Showing posts with label Tanzania na EAC. Show all posts
SERIKALI YA TANZANIA KUENDELEA KUIMARISHA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

SERIKALI YA TANZANIA KUENDELEA KUIMARISHA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

IMG_9491Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta (katikati) akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu Serikali ya Tanzania ilivyodhamiria kuimarisha ushirikiano baina yake na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Amantius Msole na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi  Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa.
IMG_9566Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta akisisitiza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu Tanzania itakavyonufaika na mfumo wa himaya moja ya forodha katika kuimarisha biashara kati ya nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.
IMG_9572
aziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam juu ya  Shirikika la ndege la Tanzania (ATCL) kupanua huduma zake na kufika Bujumbura nchini Burundi, ATCL ilianza kufanya safari zake kati ya Tanzania na Burundi Desemba16, 2013 mara tatu kwa wiki kama moja ya hatua za kuimarisha usafiri wa anga kati ya nchi wanachama. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Amantius Msole.
…………………………….
Na Frank Mvungi
Serikali ya Tanzania imedhamiria kuimarisha ushirikiano baina yake na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Nyanja za miundombinu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Mh.Sitta alibainisha kuwa mwishoni mwa mwaka 2013 Mawaziri wa Tanzania, Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) walikutana kujadili namna ya kuimarisha miundo mbinu ya barabara, reli, anga, anga na maji.
Mh.Sitta aliongeza kuwa katika kikao hicho ilikubaliwa kuwa Shirikika la ndege la Tanzania (ATCL) lipanue huduma zake na kufika Bujumbura nchini Burundi ambapo ATCL ilianza kufanya safari zake kati ya Tanzania na Burundi Desemba16, 2013 mara tatu kwa wiki kama hatua za awali za utekelezaji.
Mh. Sitta alisisitiza kuwa katika mkutano wa 8 wa Baraza la la Mawaziri la Jumuiya hiyo umeridhia mfumo wa himaya moja ya Forodha na mpangokazi unaoainisha masuala ya utekelezaji katika kipindi cha miezi sita ili kuwezesha kuanzishwa kwa himaya hiyo ifikapo Juni 2014.
Mh. Sitta akifafanua zaidi alisema mfumo wa himaya moja ya forodha unaainisha utaratibu wa mzunguko wa biashara, usimamizi wa mapato na mfumo wa kisheria.
Katika mfumo huo Sitta alisema kuwa ilikubalika kuwa nchi wanachama zitakusanya mapato yake ya kodi.
Aidha, kwa bidhaa zinazopitia nchi moja kuelekea nchi nyingine wanachama za Jumuiya hiyo zimekubaliana kuwa nchi husika itakusanya mapato yake na kuifahamisha mamlaka ya forodha mizigo ilipoingilia katika Jumuiya kwa kwa ajili ya kuruhusu bidhaa kuondoshwa.
Mkutano wa 15 wa Kawida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya Afrika Mashariki Uliofanyika Jijini Kampala, Uganda Novemba 30, 2013 na kuamua masula muhimu ya maendeleo ya Mkutano wa Jumuiya Afrika Mashariki.
Baadhi ya masuala yaliyojadiliwa na kutolewa uamuzi ni pamoja na kutiwa saini kwa Itifaki ya Umoja wa Fedha, kuidhinishwa uundwaji wa Himaya ya Umoja wa Forodha (Single Customs Territory).
Na mapukio na vijana
Uganda yakiri kulisaidia jeshi la Sudan Kusini vitani

Uganda yakiri kulisaidia jeshi la Sudan Kusini vitani

Jeshi  la  Uganda  limesema  kuwa  majeshi  yake yamejiunga  na  jeshi  la  serikali  ya  Sudan  kusini  katika vita  dhidi  ya  uasi  kwenye taifa  hilo  changa  duniani.
Msemaji  wa  jeshi  la  Uganda  luteni  kanali Paddy Ankunda  amesema  leo kuwa  majeshi  ya  uganda yanasaidiana na vikosi vya serikali ya Juba  kuwaondoa waasi  katika  mji  wa  Bor, mji  muhimu  karibu  na  mji mkuu juba ambao  umeshuhudia  mapigano  makali  tangu kuanza  kwa  mzozo  huo  katikati  ya  mwezi  uliopita nchini  Sudan  kusini. 
Maafisa  wa  Uganda  wamekuwa wakikana   kuwa  majeshi  ya  nchi  hiyo  yamejiunga  na mapigano, wakisema  majeshi  ya  Uganda  wamewekwa Sudan  kusini  kwa  ajili  ya  kufanikisha  zoezi  la kuwaondoa  raia.
Rais Yoweri  Museveni  wa  Uganda  amesema  jana  kuwa wanajeshi  wa  Uganda  wameuwawa  katika  mapigano nchini  Sudan  kusini. 
Akizungumza  katika  mkutano  mjini Angola  jana, Museveni  amesema  majeshi  ya  nchi  yake yamekuwa  yakipigana  kulisaidia  jeshi  la  serikali nchini Sudan  kusini.
Nao  wabunge  wa  Marekani  wameeleza  kufadhaishwa kwao  jana kuhusiana  na  wimbi  la  ghasia   nchini  Sudan kusini ,na kuwekea alama ya kuuliza hatua ya  marekani kuendelea  kutuma  mamilioni  ya  dola  kuisaidia  nchi hiyo.
na DW.DESwahili

TANZANIA YACHUKIZWA NA WANACHAMA WENZAKE WA 'EAC'

Tanzania yahuzunishwa na tabia ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Kenya, Uganda na Rwanda, ambazo ziliamua kuiweka pembeni Tanzania na kuunda "umoja wa nia", Rais Jakaya Kikwete aliliambia bunge Alhamisi (tarehe 7
Novemba7).
Kikwete aliwaambia watunga sheria katika hotuba ya kitaifa iliyotangwazwa na televisheni kwamba nchi wanachama tatu zimejitenga zenyewe na kujiendesha kinyume na Mkataba wa EAC na itifaki ya1999, jambo ambalo halikubaliki.
"Wameunda umoja wa nia, nani asiye na nia?" Kikwete alisema.
Kenya, Uganda na Rwanda zilikutana mwezi uliopita huko Kigali, pasipo wanachama wenzao wa EAC Tanzania na Burundi.
Watatu hao waliazimia kuhusu masula manane, lakini Tanzania inahusika zaidi na jitihada zake za kuunda kamati iliyopewa kazi ya kuandika katiba ya EAC na uamauzi wao wa kuunda umoja wa forodha, "ambao ulipaswa kujumuisha wanachama wote wa jumuiya", Kikwete alisema.
Tanzania inachangia shilingi bilioni 12 (dola bilioni 1.3) kwa mwaka kuendesha masuala ya EAC, kwa hiyo ni makosa kusema Tanzania haikutaka kuharakisha mchakato wa muungano wa EAC, raisi alisema.
Alisema nchi hizo tatu zinataka kujiwahisha kwenye hatua inayofuatia ya kuunda shirikisho kabla ya kukamilisha hatua tatu za mwanzo zinazotakiwa kisheria na mkataba na itifaki. .
"Mkataba uko wazi. Unatuwekeza kuanza na umoja wa forodha, soko la pamoja, fedha moja na baada ya hapo shirikisho," Kikwete alisema. "Tunataka kujenga msingi imara wa uchumi ambao utatoa uhakikisho wa shirikisho."
Alisema nchi wanachama wote wa EAC zilikutana Arusha tarehe 28 Aprili na kukubaliana kutoa ripoti kwenye mkutano wa wakuu wa nchi uliopangwa kufanyika tarehe 30 Novemba huko Kampala. Lakini mwezi Juni, nchi hizo tatu ziliamua kujitenga, pasipo kushirikisha Tanzania.
Hahari na Sabahi Online

Kategori

Kategori