Showing posts with label Kenya. Show all posts
Showing posts with label Kenya. Show all posts

RAIS WA KENYA AVURUGA BARAZA LA WAMAWAZIRI!


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amefanya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri na kuwapiga chini mawaziri wote ambao wizara zao zinakumbwa na kashfa za ufisadi.

Uamuzi wa Rais Kenyatta umekuja siku moja baada ya kutangaza ufisadi kama tishio la usalama wa kitaifa huku akiazimia kufanya mabadiliko makubwa kwenye ofisi ya Rais hivi karibuni.

Katika mabadiliko hayo, Kenyatta ameongeza pia idadi ya wizara kutoka 16 hadi 20 na kuongeza idara mpya chini ya wizara hiyo, kutoka idara 26 hadi 41 kwa kile alichoeleza kuwa ni kusaidia wizara kutekeleza majukumu yao bora zaidi.

Baadhi ya mawaziri walikuwa tayari wamekwisha jiondoa kwenye wizara zao kwa tuhuma za ufisadi huku wengine wakiwa na kesi za kujibu mahakamani.

Hivi karibuni, Waziri wa Ugatuzi, Anne Waiguru alikuwa wa mwisho kujiondoa kwenye wizara akiwa na kashfa zilizopata umaarufu zaidi kwa kipindi cha hivi karibuni za kununua kalamu moja kwa shilingi zaidi ya 200,000 za Tanzania.

Hata hivyo, Uhuru Kenyatta hakuwa na budi ya kuvunja baraza lake na kuunda upya kwa kuwa katiba ya nchi hiyo inataka idadi ya mawaziri isiwe chini ya 14. Baada ya Waiguru kujiuzulu nafasi ya uwaziri, baraza la mawaziri lilibaki na mawaziri 13 pekee.

RAIS WA TANZANIA ANAVYO ENZIWA NA WAKENYA

Na Francis Godwin

Unajua nini mtu wangu una kila sababu ya kujivunia kuwa Tanzania wakati na muda kama huu kwani kasi ya Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli inaweka headlines kubwa sana kwa nchi za jirani na si kwa Watanzania pekee!
Nimetembelea mtandao wa kijamii wa Twitter na nimekutana na tweets za Wakenya juu ya Rais Dk. John Pombe Magufuli na kwenye kuzisoma tweets zao nimegundua sifa za Rais Magufuli na maamuzi yake ya kazi toka ameshika rungu la Tanzania zimewafikia.
Wengi wamemsifia na wengine wameandika wakiomba Mungu awape Rais kama Magufuli….. tweets nyingine unaweza kuzisoma kwenye hii post.
MAGU
Kwa kipindi kifupi alichoingia madarakani, Rais Dk. John Magufuli amefanya mambo kadhaa ambayo yamewaridhisha na kuwapa moyo Watanzania, mambo hayo ni kama…
1. Ziara yake ya kushtukiza kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili  ilivumbua vitu vingi na kumpelekea Rais Magufuli kufuta bodi ya Wakurugenzi wa hospitali hiyo pamoja na kumuondoa Kaimu Mkurugenzi wake, Dk. Hussein Kidanto.
2. Kufuta safari za viongozi kwenda nchi za nje ili kupunguza matumizi makubwa ya pesa za Serikali.
3. Alielekeza shilingi milion 225 zilizochangwa kwa ajili ya kugharamia hafla ya Pongezi za Wabunge Dodoma kutumika kununua vitanda vya hospitali na shilingi milion 15 tu ndio zitumike kwaajili ya sherehe hiyo.
4. Jumatatu ya tarehe 23 November 2015, Rais Dk. John Magufuli alitangaza kufuta kwa sikukuu ya Uhuru December 9 na kuagiza fedha za maandalizi ya sikukuu hiyo zitumike kutatua matatizo mengine pia ameagiza siku hiyo itumike kusafisha mazingira ili kupunguza matatizo ya kipindupindu nchini.
Mambo haya machache na makubwa yamewapa faraja kubwa sana Watanzania na kumfanya Rais Magufuli awe topic kubwa kwenye mtandao wa Twitter kwa raia wa Kenya!
Kama kawaida kazi yangu ni kuzinasa zile zote zinazoweka headlines wakati huu na hizi ni baadhi ya#tweets nilizofanikiwa kuzinasa, karibu uzipitie moja baada ya nyingine uone jinsi gani Wakenyawalivyoguswa…
MAGU11
>>> “Magufuli aje atoe lock ya Uhuru kwani yeye ni Pombe“. <<< @Danielki_
MAGU2
>>> Uhuru Kenyatta inabidi aazime ujuzi kutoka kwa mwenzake wa Tanzania, Magufuli!!!“<<< @Fifi.
>>>Magufuli chini ya mwezi mmoja madarakani vs. Uhuru zaidi ya miaka 2.5 madarakani. #stateofthenation“.<<< @ShadrackMusyoki.
MAGU3
>>> “#StateOfTheNation Magufuli alianza na kasi ya vitendo akiwa na siku 2 madarakani, miaka 3 imepita na Uhuru bado anatengeneza mabaraza ya kumsaidia kufanya kazi“<<<  @MafisiPope
>>> “Rais Uhuru amekuwa akiongea toka mwaka 2013, Rais Magufuli amekuwa akifanya kwa VITENDO toka wiki 3 zilizopita. Matunda zaidi yamepatikana ndani ya  vitendo vya wiki 3 kuliko porojo za miaka 3“. <<< @CollinsFabien.
MAGU4
>>> “Wakati Watanzania wanaamka kutokana na kile Magufuli alichokifanya, Wakenya wanaamka kwa kile alichokiahidi Uhuru @Ma3Route“. <<< MuthuiMkenya.
>>> “Rais Uhuru Kenyatta inabidi afanye kwa vitendo na aache kuzungumza. Tunataka tumuone akitenda kama Buhari, na Magufuli. Ameshaongea vya kutosha! Tenda sasa!!” <<< GeorgeOnyango.
MAGU5
>>> “Wakenya inabidi wachukue somo kutoka kwa Magufuli! Huyu jamaa ana porojo chache & vitendo vingi“. <<< @Blueprint.
>>> “Kwa kuwa Wakenya wanamtaka sana Magufuli, tunaweza tukafikiria kuigeuza Kenya kuwa moja ya mikoa yetu“. <<< @Magembe.
MAGU6
>>> “Magufuli atatimiza, Buhari atatimiza. Kenya tunahitaji jamii ya vitu hivi viwili. labda tujaribu na Mashirima Kapombe pengine majina ya ajabu yatafanya kazi“. <<< @mathaland.
>>> “Magufuli ametimiza vingi zaidi ndani ya wiki mbili kuliko miaka mitatu ya Serikali ya Kenya“. <<< @labokaigi.
MAGU7
>>> “Laiti Kenya ingekuwa na Magufuli“. <<< @Mwanthi.
>>> “Magufuli inabidi aje awe na Rais wa Kenya bana…” <<< @kubz_bomaye.
MAGU8
>>> “Tunaweza tukapata msaidizi wa Magufuli Kenya tafadhali?” <<< @alawiabdul.
>>> “Rais Magufuli yupo serious na kupunguza matumizi. Kenya inabidi wajifunze kitu hiki“. <<< @OriemaOduk.
MAGU9
>>> “MUNGU tafadhali ibariki Kenya na Rais kama wa Tanzania, Rais Magufuli“. <<< @sandie_swat.
>>> “Sasa hivi nashawishika kupita kiasi kuamini kuwa Kenya inahitaji Rais kutoka kwenye kundi dogo la watu ambalo hatujawahi kulisikia kama vile alivyo Magufuli kwa Tanzania.” <<< @anita.
MAGU10
>>> “Wakati Wabunge wa Kenya wanamsindikiza DP kwenda The Hague, ona alichokifanya Magufuli… “. <<< @ButterCup
>>> “Kenya na Tanzania inabidi waungane ili Magufuli awe Rais wetu pia. ” <<< @Mungai.

JIONI YA LEO PAPA FRANCIS ATUA KENYA IKIWA NI NCHI YA KWANZA AFRIKA KUTEMBELEWA NA KIONGIZI HUYO


Rais Uhuru Kenyatta akisalimiana na kumpokea Kiongozi wa kanisa la katoliki duniani Papa Francis muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa JKIA nchini Kenya jioni hii
Kikwete ahutubia bunge la Kenya

Kikwete ahutubia bunge la Kenya


Rais Kikwete waTanzania
Rais Kikwete waTanzania
Rais Jayaka Kikwete wa Tanzania amehutubia mabaraza mawili ya Bunge la Kenya mjini Nairobi Jumanne alasiri na kusema uhusiano kati ya Kenya na Tanzania utaendelea kuimarika zaidi na uongozi ujao wa Tanzania.
Rais Kikwete aliwasili katika majengo ya bunge Nairobi mwendo wa saa tisa na dakika 40 na kulakiwa na kundi kubwa la wabunge na wanachama wa Baraza la Senate waliokuwa na hamu ya kumsikiliza kiongozi huyo wa Tanzania anayetarajiwa kustaafu kwenye uongozi baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Tanzania tarehe 25 mwezi huu.

Kulikuwa na ulinzi mkali katika majengo ya bunge na wabunge wa chama tawala na wale wa upinzani walimiminika kwa wingi ndani ya majengo ya Bunge.
Baadaye Rais Kikwete aliwahutubia wabunge na kusema ni siku 19 kabla ya uchaguzi mkuu Tanzania na alialikwa na Rais Kenyatta kufika Kenya kuwaaga raia wa Kenya. Amesema Kenya ni rafiki na mshiriki mkubwa wa Tanzania. Amesema baada ya mkasa na ghasia za uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 nchini Kenya alifika mara moja hapa Nairobi kutatua mzozo huo bila kualikwa isipokuwa kwa yeye mwenyewe kuomba kwenda Kenya kusaidia kupata ufumbuzi.
Ziara ya Rais Kikwete hapa Nairobi imekuwa na shughuli nyingi. Gavana wa jiji kuu la Nairobi Evans Kidero amemtunukia Rais Kikwete heshima kuu kwa kumkabidhi ufunguo maalum kama ishara ya mtu huru mjini Nairobi. Pia barabara mashuhuri ya Milimani imebadilishwa jina na kupewa jina la Jakaya Kikwete Road.

Mgomo Kenya; Walimu Waigomea Mahakamaโ€ฆ!

Mgomo Kenya; Walimu Waigomea Mahakama…!


Moja ya madarasa yakiwa tupu kutokana na mgomo wa walimu unaoendelea nchini Kenya.
Moja ya madarasa yakiwa tupu kutokana na mgomo wa walimu unaoendelea nchini Kenya.

UFUNDISHAJI masomo anuai katika shule za umma nchini Kenya umekwama licha ya amri ya mahakama ya kuwataka walimu ikilazimisha warejee shuleni Jumatatu. Mgomo wa walimu nchini Kenya umeingia wiki ya tano hivi sasa huku ufundishaji ukiendelea kuathirika.
Vyama vya walimu nchini Kenya vimesema havitatekeleza amri ya mahakama iliyowataka kusitisha mgomo huo kwa siku tisini kuanzia leo. Badala yake vyama hivyo vimerejea mahakamani leo kutaka ufafanuzi zaidi kuhusu uamuzi huo.
Hata hivyo kesi yao iliahirishwa hadi alhamisi wiki hii. Walimu walijitokeza kwa wingi wakiandamana na viongozi wao wa vyama vya walimu mwendo wa saa nane unusu. Walimu walikwenda mahakamani kutafuta ufafanuzi kuhusu ratiba ya mihula ambayo serikali ilibadilisha hapo awali mgomo ulipochacha.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi siku ya Alhamisi saa nane u nusu kwa sababu jaji aliyekuwa akisikiza kesi hiyo aliomba radhi iliapokee matibabu. Jijini Nairobi hii leo shule ya Msingi ya Moi Avenue na Shule ya Msingi ya Nairobi hazikuwa na wanafunzi. Wanafunzi wamesalia nyumbani huku walimu wakiwa wamegoma kurejea shuleni kama walivyoagizwa na mahakama ya nchi hiyo.
-BBC

I Hate Kenyans With a Passion & I’ll Deport Them From US - DONALD TRUMP Tells BBC.

US real estate magnate and Republican Presidential candidate, Donald Trump, has again hit out at Kenyans terming them as fraudsters and conmen.

Responding to a Kenyan journalist who works with the BBC, Trump said that he hates Kenyans with a passion because they are opportunists like US President Barrack Obama, who is a Kenyan-American.

“Sir, my name is Gladys, a Kenyan journalist working for BBC; Kenyans have complained that you hate them and that recently you called our athletes that won in Beijing cheap frauds and conmen. Do you still hold that position and if so, why do you hate us so much Mr. Trump?” Gladys asked.

“I hate Kenyans starting with Obama and that is why I promise to deport all of them when I ascend to the helm. You people sneaked into our country and you’ve devalued it greatly. Look at this clown that calls himself POTUS, this one has rendered America to the dogs and it is time we made our beloved country great again. Recently I heard that you people have generated twitter hashtags trying to rebuke me. I am the pillar of America, a true American and any Kenyan that feels irritated can go to hell or call me directly if he has the balls to do so. I will put all of them including you, in their rightful positions” Trump responded.

Kategori

Kategori