Na Francis Godwin
Unajua nini mtu wangu una kila sababu ya kujivunia kuwa Tanzania wakati na muda kama huu kwani kasi ya Rais wetu Dk. John Pombe Magufuli inaweka headlines kubwa sana kwa nchi za jirani na si kwa Watanzania pekee!
Nimetembelea mtandao wa kijamii wa Twitter na nimekutana na tweets za Wakenya juu ya Rais Dk. John Pombe Magufuli na kwenye kuzisoma tweets zao nimegundua sifa za Rais Magufuli na maamuzi yake ya kazi toka ameshika rungu la Tanzania zimewafikia.
Wengi wamemsifia na wengine wameandika wakiomba Mungu awape Rais kama Magufuli….. tweets nyingine unaweza kuzisoma kwenye hii post.
Kwa kipindi kifupi alichoingia madarakani, Rais Dk. John Magufuli amefanya mambo kadhaa ambayo yamewaridhisha na kuwapa moyo Watanzania, mambo hayo ni kama…
1. Ziara yake ya kushtukiza kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili ilivumbua vitu vingi na kumpelekea Rais Magufuli kufuta bodi ya Wakurugenzi wa hospitali hiyo pamoja na kumuondoa Kaimu Mkurugenzi wake, Dk. Hussein Kidanto.
2. Kufuta safari za viongozi kwenda nchi za nje ili kupunguza matumizi makubwa ya pesa za Serikali.
3. Alielekeza shilingi milion 225 zilizochangwa kwa ajili ya kugharamia hafla ya Pongezi za Wabunge Dodoma kutumika kununua vitanda vya hospitali na shilingi milion 15 tu ndio zitumike kwaajili ya sherehe hiyo.
4. Jumatatu ya tarehe 23 November 2015, Rais Dk. John Magufuli alitangaza kufuta kwa sikukuu ya Uhuru December 9 na kuagiza fedha za maandalizi ya sikukuu hiyo zitumike kutatua matatizo mengine pia ameagiza siku hiyo itumike kusafisha mazingira ili kupunguza matatizo ya kipindupindu nchini.
Mambo haya machache na makubwa yamewapa faraja kubwa sana Watanzania na kumfanya Rais Magufuli awe topic kubwa kwenye mtandao wa Twitter kwa raia wa Kenya!
Kama kawaida kazi yangu ni kuzinasa zile zote zinazoweka headlines wakati huu na hizi ni baadhi ya#tweets nilizofanikiwa kuzinasa, karibu uzipitie moja baada ya nyingine uone jinsi gani Wakenyawalivyoguswa…
>>> “Magufuli aje atoe lock ya Uhuru kwani yeye ni Pombe“. <<< @Danielki_
>>> “Uhuru Kenyatta inabidi aazime ujuzi kutoka kwa mwenzake wa Tanzania, Magufuli!!!“<<< @Fifi.
>>>“Magufuli chini ya mwezi mmoja madarakani vs. Uhuru zaidi ya miaka 2.5 madarakani. #stateofthenation“.<<< @ShadrackMusyoki.
>>> “#StateOfTheNation Magufuli alianza na kasi ya vitendo akiwa na siku 2 madarakani, miaka 3 imepita na Uhuru bado anatengeneza mabaraza ya kumsaidia kufanya kazi“<<< @MafisiPope
>>> “Rais Uhuru amekuwa akiongea toka mwaka 2013, Rais Magufuli amekuwa akifanya kwa VITENDO toka wiki 3 zilizopita. Matunda zaidi yamepatikana ndani ya vitendo vya wiki 3 kuliko porojo za miaka 3“. <<< @CollinsFabien.
>>> “Wakati Watanzania wanaamka kutokana na kile Magufuli alichokifanya, Wakenya wanaamka kwa kile alichokiahidi Uhuru @Ma3Route“. <<< MuthuiMkenya.
>>> “Rais Uhuru Kenyatta inabidi afanye kwa vitendo na aache kuzungumza. Tunataka tumuone akitenda kama Buhari, na Magufuli. Ameshaongea vya kutosha! Tenda sasa!!” <<< GeorgeOnyango.
>>> “Wakenya inabidi wachukue somo kutoka kwa Magufuli! Huyu jamaa ana porojo chache & vitendo vingi“. <<< @Blueprint.
>>> “Kwa kuwa Wakenya wanamtaka sana Magufuli, tunaweza tukafikiria kuigeuza Kenya kuwa moja ya mikoa yetu“. <<< @Magembe.
>>> “Magufuli atatimiza, Buhari atatimiza. Kenya tunahitaji jamii ya vitu hivi viwili. labda tujaribu na Mashirima Kapombe pengine majina ya ajabu yatafanya kazi“. <<< @mathaland.
>>> “Magufuli ametimiza vingi zaidi ndani ya wiki mbili kuliko miaka mitatu ya Serikali ya Kenya“. <<< @labokaigi.
>>> “Laiti Kenya ingekuwa na Magufuli“. <<< @Mwanthi.
>>> “Magufuli inabidi aje awe na Rais wa Kenya bana…” <<< @kubz_bomaye.
>>> “Tunaweza tukapata msaidizi wa Magufuli Kenya tafadhali?” <<< @alawiabdul.
>>> “Rais Magufuli yupo serious na kupunguza matumizi. Kenya inabidi wajifunze kitu hiki“. <<< @OriemaOduk.
>>> “MUNGU tafadhali ibariki Kenya na Rais kama wa Tanzania, Rais Magufuli“. <<< @sandie_swat.
>>> “Sasa hivi nashawishika kupita kiasi kuamini kuwa Kenya inahitaji Rais kutoka kwenye kundi dogo la watu ambalo hatujawahi kulisikia kama vile alivyo Magufuli kwa Tanzania.” <<< @anita.
>>> “Wakati Wabunge wa Kenya wanamsindikiza DP kwenda The Hague, ona alichokifanya Magufuli… “. <<< @ButterCup
>>> “Kenya na Tanzania inabidi waungane ili Magufuli awe Rais wetu pia. ” <<< @Mungai.