Showing posts with label 2017 at 10:31AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 10:31AM. Show all posts
Ndugai: Hamna Cha Kesi, Mimi Ndio Spika Watakaa Benchi Mwaka Mzima

Ndugai: Hamna Cha Kesi, Mimi Ndio Spika Watakaa Benchi Mwaka Mzima

Mahakama zetu zimeendelea kudharaulika baada ya leo bungeni spika ndugai kusema wabunge waliosimamishwa vikao mwaka mzima wanakimbia kimbia tu hakuna cha kesi mimi ndio Spika.
Nimejiuliza,Ndugai anahakika gani kama mahakama itaamua tofauti na maamuzi yake ya kuwasimamisha mwaka?
Je,Ina maana Ndugai anauwezo wa kuingilia maamuzi ya mahakama mpaka kujipiga kifua hamna cha kesi?”Na kejeli”
Kauli kama hizi endapo mahakama itaamua kuendana na majigambo ya Spika ndugai hata kama maamuzi yake yatakuwa ya haki,zinapunguza imani ya wananchi kwa mahakama zao.Lazima mahakama ijipange la sivyo hadhi yake inaweza kuporomoka kabisa.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tuIBWS
via IFTTT


Jeshi la Polisi Dar kuhusu ulinzi na usalama kwenye mechi za Ndondo Cup 2017

Jeshi la Polisi Dar kuhusu ulinzi na usalama kwenye mechi za Ndondo Cup 2017

Jeshi la polisi limethibitisha kuungana na wadau wa soka mkoa wa Dar es Salaam katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa wachezaji, viongozi, waamuzi, mashabiki na mali zao wakati wote wa mashindano ya Ndondo Cup 2017.
Kamisha msaidizi wa polisi (ACP) Philip Kalangi amesema, jeshi la polisi litatumia mbinu ya ulinzi shirikishi pamoja na wadau wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha amani inakuwepo wakati wote wa mashindano.
“Tumejipanga lakini tutakuwa na ullinzi shirikishi ambao utahusisha wadau wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama na vikundi mbalimbali vya ulinzi navyo vitakuwepo. Tunawasihi wananchi wajitokeze kwa wingi kuja kuona vijana wao, wapate burudani na mwisho wa siku tupate kitu tunachokitarajia.”
“Suala la ulinzi na usalama ni muhimu sana katika jambo lolote kwenye maisha ya kila siku, ulinzi na usalama ni suala mtambu na linahitaji ushirikishwaji wa pamoja, makuindi yote katika jamii yetu tunatakiwa tushiriki katika nafasi yake linahitaji kushiriki moja kwa moja katika ulinzi na usalama.”
“Hata kwenye jeshi la polisi tunafanya michezo, tuna program moja inaitwa michezo na vijana ambapo tumekuwa tunahamasisha vijana kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya na uhalifu wa aina mbalimbali.”
“Kama mnavyofahamu, michezo inajenga ushirikiano, upendo na mambo mengi lakini kubwa ni ajira. Vijana wengi hawana ajira kwa hiyo kwenye mashindano haya tunategemea vipaji mbalimbali vitaibuliwa na kuwasaidia hapo badae kwenye maisha yao.”
“Sisi kama jeshi la polisi tutakuwepo na tumekuwa na mahusiano na raia enzi na enzi tangu kuanzishwa kwa jeshi la poilisi, hauwezi kututenga na raia wala huwezi kuwatenga raia na askari. Kwa hiyo ushirikiano ni lazima uwepo na uendelee kwenye masuala ya ulinzi na usalama.”
Michuano ya Ndondo Cup 2017 hatua ya makundi inataraji kuanza rasmi Jumamosi Juni 17, 2017 ambapo mechi ya ufunguzi wa hatua ya makundi itazikutanisha Stimtosha dhidi ya Makuburi kwenye uwanja wa Kinesi.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rpqmBX
via IFTTT


Tetesi za usajili Jumanne ya leo, Ranieri apata timu mpya.

Tetesi za usajili Jumanne ya leo, Ranieri apata timu mpya.

Baada ya kuipandisha ligi kuu kocha Claudio Ranieri aliipa Leicester ubingwa wa Epl lakini msimu uliofuata alitimuliwa na timu hiyo, lakini leo kocha Claudio Ranieri amepata klabu mpya baada ya timu ya Nantes ya nchini Ufaransa kumtambulisha kama kocha wao mpya.
Lakini huko huko nchini Ufaransa klabu ya Psg imeionya klabu ya Barcelona kuhusu kiungo wao Marco Veratti na kusisitiza kwamba kiungo huyo hauzwi kwa dau lolote hivyo Barcelona wakatafute mchezaji mwingine.
Klabu ya Arsenal ambayo inamsaka kwa udi na uvumba mshambuliaji wa Lyon Alexandre Lacazette, sasa klabu ya Lyon imetaja dau ambalo Arsenal wanapaswa kulipa kama wanamtaka itabidi watoe euro 48.7m.
Baada ya kutoswa na kocha George Sampaoli aliyepata kazi mpya ya kuinoa timu ya taifa ya Argentina, klabu ya Sevilla leo imepata kocha mpya ambapo aliyekuwa kocha wa Celta bwana Edurdo Berizzo amepewa jukumu hilo la Sampaoli.
Mshambuliaji raia wa Crotia Ivan Perisic ambaye anawindwa sana na klabu ya Manchester United inasemekana amewaambia wazi waajiri wake klabu ya Inter Milan kwamba wamuache ajiunge na Manchester United.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2s9kXwd
via IFTTT


Matokeo ya michezo mikubwa ya kirafiki hii leo.

Matokeo ya michezo mikubwa ya kirafiki hii leo.

Timu ya taifa ya Brazil ikiwa ugenini dhidi ya Australia ilitoa kipigo kikubwa cha mabao 4 kwa 0 dhidi ya Australia huku mabao ya Brazil yakiwekwa kambani na Diego Souza, Thiago Silva, Taison na Diego Souza.
Argentina nao walikuwa ugenini dhidi ya Singapore walishinda mabao 6 kwa 0 huku mabao ya Argentina yakifungwa na Fredrico Fazio na Joaquin Correa waliofunga kipindi cha kwanza huku kipindi cha pili yaliongezwa mengine manne Gomez,Daniel Parades,Lucas Alario na Di Maria.
Waafrika wenzetu Bafanabafana walikuwa nyumbani kuikaribisha Zambia na Zambia waliibuka kidedea kwa ushindi wa mabao mawili kwa moja huku mabao ya Zambia yakiwekwa kimiani na Brian Mwila na Lubinda Munia huku la kufutia machozi la Bafanabafana likifungwa na Lebongang Manyama.
Mabingwa wa Afrika timu ya taifa ya Cameroon walifungwa mabao 4 kwa 0 na Colombia huku mabao ya Colombia yakifungwa na Rodriguez,Yery Moina akifunga mawili na Jose Izquirero huku Cameroon wakimaliza pungufu baada ya Ndip Tambe kupewa kadi nyekundu.
Mabao mawili ya Harry Kane hayakutosha kuizuia England isifungwe mabao 3 kwa 2 na Ufaransa ambao mabao yao yalifungwa na Samuel Umtiti,Djibrii Sidibe na Osmane Dembele katika mchezo ambao Ufaransa walimaliza pungufu baada ya Raphael Varane kuoneshwa kadi nyekundu,
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rq7D9t
via IFTTT


Sumaye Aibuka na Kuinyooshea Kidole Serikali ya Magufuli..Adai Haitafanya Jambo Lolote la Maana kwa Sababu Hii..!!

Sumaye Aibuka na Kuinyooshea Kidole Serikali ya Magufuli..Adai Haitafanya Jambo Lolote la Maana kwa Sababu Hii..!!

WAZIRI Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Fredrick Sumaye, alisema nchi inashindwa kuendelea kwa sababu inaendeshwa kwa ushabiki wa kisiasa hata katika masuala yenye masilahi kwa Taifa.
Sumaye aliyasema hayo mwishoni mwa wiki kwenye kongamano la Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (Bavicha) pamoja na Umoja wa Vijana wa
Vyuo Vikuu ambao ni wanachama wa chama hicho jijini Mbeya (Chaso)
Sumaye ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema mambo mengi yenye masilahi ya
Taifa hayapaswi kufanyiwa mzaha kwani yanaweza kuzusha madhara makubwa ambayo hayakutarajiwa.
Sumaye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, alitolea mfano suala la bajeti ya mwaka huu 2017/2017 kwamba inaonyesha wazi haina uhalisia wa maisha ya wananchi wa kipato cha chini ambao ni wengi.
Alisema bajeti hiyo ingechambuliwa vyema na chombo chenye uwakilishi wa wananchi yaani Bunge kama chombo huru, lakini katika miaka ya hivi karibuni limeingiliwa na Serikali ya chama tawala na hivyo kupoteza sifa yake ya kuwasimamia wananchi.
“Nchi kwa sasa inayumba na inashindwa kuendelea kutokana na kuendeshwa kishabiki, bajeti yetu ya mwaka uliopita fedha za miradi ya maendeleo
zilitolewa kwa asilimia 34 pekee na Serikali ilikiri, lakini sasa hivi wanakuja na bajeti kubwa zaidi ya hiyo ambayo haijatekelezwa na wabunge wa CCM wanashangilia,” alisema Sumaye na kuongeza:
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2s9lC0z
via IFTTT


Mashabiki wa Timu ya Gor Mahia ya Kenya Wamtaka Magufuli Kumpiga โ€˜Tafuโ€™ Raila Odinga Kwenye Uchaguzi Mkuu wa Kenya..!!

Mashabiki wa Timu ya Gor Mahia ya Kenya Wamtaka Magufuli Kumpiga ‘Tafu’ Raila Odinga Kwenye Uchaguzi Mkuu wa Kenya..!!

Wakati Gor Mahia ikiibuka na ushindi wa bao 3 0 dhidi ya AFC Leopard katika michuano ya SportPesa SuperCup ambapo watani hawa wa jadi kutoka Kenya walipokutana Tanzania, shabiki wa timu hiyo amemuomba Magufuli kutoa msaada kwa Raila Odinga.
Jenerali Jaro Soja ambaye ni Rais wa mashabiki wa Gor Mahia amemuomba Rais Magufuli kumsaidia mlezi wa timu yao hiyo Mhe. Raila Odinga katika kampeni zake kama ambavyo kiongozi huyo alifanya kipindi Tanzania inafanya uchaguzi mkuu mwaka 2015 ambapo Raila Odinga alikuwa akimpa nguvu Rais John Pombe Magufuli. 
Jaro Soja anasema kuwa wao kama mashabiki wa Gor Mahia wanampenda sana Rais Magufuli kwa kuwa yeye ni rafiki mkubwa wa mlezi wao wa timu hivyo wanamkaribisha Kenya. 
Credit – EATV
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rq02Yz
via IFTTT


Kategori

Kategori