Jeshi la Polisi Dar kuhusu ulinzi na usalama kwenye mechi za Ndondo Cup 2017

Jeshi la polisi limethibitisha kuungana na wadau wa soka mkoa wa Dar es Salaam katika kuhakikisha ulinzi na usalama wa wachezaji, viongozi, waamuzi, mashabiki na mali zao wakati wote wa mashindano ya Ndondo Cup 2017.
Kamisha msaidizi wa polisi (ACP) Philip Kalangi amesema, jeshi la polisi litatumia mbinu ya ulinzi shirikishi pamoja na wadau wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha amani inakuwepo wakati wote wa mashindano.
“Tumejipanga lakini tutakuwa na ullinzi shirikishi ambao utahusisha wadau wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama na vikundi mbalimbali vya ulinzi navyo vitakuwepo. Tunawasihi wananchi wajitokeze kwa wingi kuja kuona vijana wao, wapate burudani na mwisho wa siku tupate kitu tunachokitarajia.”
“Suala la ulinzi na usalama ni muhimu sana katika jambo lolote kwenye maisha ya kila siku, ulinzi na usalama ni suala mtambu na linahitaji ushirikishwaji wa pamoja, makuindi yote katika jamii yetu tunatakiwa tushiriki katika nafasi yake linahitaji kushiriki moja kwa moja katika ulinzi na usalama.”
“Hata kwenye jeshi la polisi tunafanya michezo, tuna program moja inaitwa michezo na vijana ambapo tumekuwa tunahamasisha vijana kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya na uhalifu wa aina mbalimbali.”
“Kama mnavyofahamu, michezo inajenga ushirikiano, upendo na mambo mengi lakini kubwa ni ajira. Vijana wengi hawana ajira kwa hiyo kwenye mashindano haya tunategemea vipaji mbalimbali vitaibuliwa na kuwasaidia hapo badae kwenye maisha yao.”
“Sisi kama jeshi la polisi tutakuwepo na tumekuwa na mahusiano na raia enzi na enzi tangu kuanzishwa kwa jeshi la poilisi, hauwezi kututenga na raia wala huwezi kuwatenga raia na askari. Kwa hiyo ushirikiano ni lazima uwepo na uendelee kwenye masuala ya ulinzi na usalama.”
Michuano ya Ndondo Cup 2017 hatua ya makundi inataraji kuanza rasmi Jumamosi Juni 17, 2017 ambapo mechi ya ufunguzi wa hatua ya makundi itazikutanisha Stimtosha dhidi ya Makuburi kwenye uwanja wa Kinesi.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rpqmBX
via IFTTT