VIDEO: NJOMBE MJI YAICHAKAZA AZAM 2-0

Leo July 24 2017 kulikuwa na mchezo wa maandalizi ya msimu mpya 2017/2018 kati ya Klabu kutoka Dar es Salaam Azam Fc dhidi ya wenyeji Njombe Mji Fc ambayo imepanda Ligi kuu msimu ujao.
Katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Aman Makambako umbali takribani kilometa 60 kutoka Njombe mjini ulishuhudiwa na mashabiki wengi sana mkoani humo kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa bila kushuhudia timu kubwa mkoani humo.
NjombeMji Fc wameonyesha kuwa kile kilichokuwa kinazungumzwa juu ya usajili wao wa mashaka kuwa walikuwa kimya lakini wachezaji wenye uwezo wa kucheza Ligi Kuu wapo.
Katika mchezo huo Njombe wakafanikiwa kuwafunga Azam Fc jumla ya magoli 2-0 mabao ambayo yaliwekwa kambani na Nyota kutoka Nchini Nigeria Adam Baiko na Siame aliyeshindilia msumari wa mwisho dakika ya 80.
SokaOnline ilifanikiwa kunasa magoli ambayo yalifungwa kwenye mchezo huo angalia hapa chini.

from Blogger http://ift.tt/2uqwCJP
via IFTTT