‘Uthibiti wa uhalifu mitandaoni bado ni TATIZO’

Tanzania haina uwezo wa kudhibiti uhalifu wa kimtandao kutokana na mitandao inayotumika kumilikiwa na watu wa Magharibi.
Kauli hiyo imetolewa wiki hii katika mkutano uliowakutanisha viongozi wa Serikali kutoka Tanzania na China na wawakilishi wa vyombo vya habari jana.
Image result for mitandaoni
Mkutano huo ulikuwa ukidhibiti matumizi mabaya ya mtandao yanayoweza kuleta madhara katika vyombo vya habari.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani amesema sheria ya udukuzi wa kimtandao inayotumika nchini haina uwezo wa kuwawajibisha watu wanaotumia vibaya mtandao kutokana na tofauti za tamaduni.
“Sasa tuna watu wanaodhibiti wahalifu wa kimtandao, lakini wanapata wakati mgumu kuthibitisha ushahidi kupitia mitandao ya kijamii kwa sababu mingi inatoka Marekani na kusimamiwa na sheria za nchi hiyo,” amesema Ngonyani.
Balozi wa China nchini, Lu Youqing amesema Tanzania ni moja kati ya nchi barani Afrika ambayo matumizi ya kimtandao yanakua kwa kasi, hivyo ni lazima kuwe na udhibiti wa watumiaji wabaya.
“Kupitia takwimu za TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania) zinaonyesha kuna ongezeko la mara 13.7 kwa watumiaji wa simu ndani ya miaka 10 kutoka milioni 2.9 mwaka 2005 hadi kufikia watu milioni 39.8 mwaka 2015, huku watumiaji wa tovuti wakifikia milioni 17.26 mwaka 2015 kutoka milioni 1.01 mwaka 2005,” amesema Balozi Youqing.

from Blogger http://ift.tt/2uJ644O
via IFTTT