Klabu ya Liguu ya soka nchini Uingereza, Everton imewasili salama katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere saa nne asubuhi ya leo kwa ajili ya mchezo wao wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya Barclays dhidi ya klabu ya Gor Mahia utakaopigwa kesho kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Klabu hiyo imetumia ndege binafsi kutoka Uingereza mpaka Dar es salaam ambapo wamepata mapokezo makubwa kutoka kwa mashabiki wa soka nchini, hasa wanaofatilia kwa karibu ligi kuu ya Uingereza na mchezaji mashuhuri aliyehamia klabu hiyo wiki iliyopita kutokea kwa Mashetani wa jijini Manchester, Wayne Rooney.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameongoza umati mkubwa wa mashabki wa soka waliojitokeza uwanja wa ndege asubuhi hii kuilaki timu ya Everton, jambo lililowafurahisha sana timu nzima ya wakali hao wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Katika tovuti ya klabu ya Everton, kikosi hicho kimeelezea kufurahishwa kwake na mapokezi makubwa waliyoyapata kutoka kwa ngoma za kabila la Kimasai na wananchi waliojitokeza kuwapokea na kwamba wachezaji wakikosi hicho wana hamasa kubwa ya kuona vivutio vya Tanzania kwa siku chache zijazo watakazokuwa hapa nchini.
Katika tovuti ya klabu hiyo, Everton wameandika:
“Tumepata mapokezi makubwa sana, ni jambo la kuvutia sana kwetu tulipopokewa na Wamasai. Ni jambo ambalo hatuwezi kabisa kuliona huko kwetu. Tumeshuka moja kwa moja kutoka kwenye ndege na sote tunafurahi sana kuwa hapa.””Tutafanya mazoezi leo usiku na tunausubiri kwa hamu mchezo wetu wa kesho. Lakini kwa sasa tutapimana ubavu tu kwakuwa tumerudi kutoka kambini wiki iliyopita tu. Itakuwa ni mchezo mzuri kwa kujipima nguvu na ni mategemeo yetu kwamba mashabiki wa hapa watajitokeza kwa wingi na wataufurahia mchezo huo.”Klabu hiyo itamenyena na Gor Mahia kesho Alhamis saa 11 jioni katika mchezo huo wa kirafiki. Gor Mahia imefanikiwa kupata nafasi hii baada ya Kampuni ya Bahati Nasibu za Michezo (SportPesa) kuendesha ligi ndogo iliyolenga kupata mshindani wa Everton. Klabu zote za Tanzania zilizoshiriki kwenye ligi hiyo zilitolewa na zote zitabaki kuwa watazamaji.
Tazama picha za mapokezi ya klabu ya Everton iliyowasili nchini leo hii:
Shabiki mnazi wa timu hiyo aliyetangulia kuja nchini siku chache zilizopita, Andrew Pemberton ameposti kwenye akaunti yake ya mtandao wa Twitter akiwaambiwa wenzake kwamba:
“Nimeipeperusha vyema bendera ya Everton nchini Tanzania kwahiyo natumai wenzangu mtanendelea pale nilipoishia mimi.”
Ujumbe huo ameuandika akiweka picha ambayo amepiga akiwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro. Mlima mrefu kuliko yote barani Afrika ambapo alipiga picha hito akiwa ameshika bendera ya klabu yake.
Kikosi cha Eveton chenye wachezaji 25 kilichowasili leo ni:
Maarten Stekelenburg, Mateusz Hewelt, Chris Renshaw, Tom Davies, Phil Jagielka, Ashley Williams, Callum Connolly, Jonjoe Kenny, Michael Keane, Muhamed Besic, Leighton Baines, Morgan Schneiderlin, James McCarthy, Davy Klaassen, Gareth Barry, Idrissa Gana Gueye, Joe Williams, Kieran Dowell, Kevin Mirallas, Wayne Rooney, Aaron Lennon, Dominic Calvert-Lewin, Ademola Lookman, Matthew Pennington, Yannick Bolasie.
from Blogger http://ift.tt/2udEazH
via IFTTT