STARS KWENDA KIGALI MCHANA HUU KUZICHAPA NA RWANDA JUMAMOSI

Kikosi cha timu ya Taifa ya mpira wa miguu Tanzania (Taifa Stars), kinakwea pipa leo mchana kwenda jijini Kigali, Rwanda kutafuta nafasi ya kushiriki mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN)
Taifa Stars inaenda Kigali ikitokea jijini Mwanza ilipoweka kambi kabla ya kucheza mchezo wa kwanza dhidi ya Rwanda Jumamosi iliyopita, itapitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere kwenda Rwanda.
Stars itaondoka Mwanza saa nne asubuhi na kuwasili Dar es Salaam majira ya saa sita mchana kabla ya kuunganisha ndege ya Rwanda majira ya saa nane alasiri kwenda Kigali.
Inakwenda Kigali kwa ajili ya mchezo wa marudiano na Rwanda maarufu kama Amavubi kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) zitakazofanyika nchini Kenya mwakani.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. Mshindi wa jumla katika michezo miwili atakuwa amesonga mbele hivyo kukutana na Uganda mwezi ujao.
Katika mchezo huo, Stars itacheza bila beki Shomari Kapombe aliyeumia mguu katika mchezo kwanza uliopigwa jijini Mwanza.

from Blogger http://ift.tt/2tp8uZ4
via IFTTT