PICHA: TAZAMA JINSI RICK ROSS ALIVYOPUNGUA UNENE

Mwanamuziki wa hip hop wa nchini Marekani Rick Ross kwa sasa amepungua unene ambao mashabiki wake wengi walizoea kumuona na yawezekana kwa baadhi ya watu ambao hawajaona picha zake kwa muda mrefu, sasa watashangazwa kwa mabadiliko makubwa aliyonayo.
“Sasa hivi nimekuwa nakula vizuri, nafanya mazoezi na kuhakikisha nakuwa fiti muda wote na bado najisikia furaha na muonekano wangu kama kawaida,” alisema Ross kuliambia jarida la ‘PEOPLE.’
Ross amesema kwamba kupungua unene kumefanya ajisikie “vizuri zaidi ya ilivyokuwa mwanzo.”
Mwanzo, Rick Ross alilazimika kupungua zaidi ya kilo 34 alipoambiwa na daktari wake kufanya hivyo baada ya viungo vyake vya mwili kupooza ghafla ndani ya kipindi cha saa mbili tu toka apate tukio hilo mwaka 2011. Kabla ya kushauriwa kufanya hivyo, Ross alikuwa na uzito wa kilo 159 ambao ndio uzito mkubwa zaidi aliowahi kuwa nao maishani. Alianza kufanya mabadiliko yaliyosaidia kupungua unene.
Rick Ross ambaye mwanzo alikuwa akipenda kuonesha ubabe kutokana na ukubwa wa mwili wake, sasa anafurahiwa na wengi hasa walio wanene sana kwa kuwahamasisha kupungua na kufikia mafanikio yake.
“Nafurahi sana, bado naendelea kupunguza unene na sasa naanza kuongeza misuli badala ya minyama uzembe.”
Tazama picha zifuatazo kuona mabadiliko hayo:
C

from Blogger http://ift.tt/2udUeB6
via IFTTT