MSAFARA WA RAIS MUGABE WAPATA AJALI

Mke wa Rais wa Zimbabwe, Grace Mugabe alipata majeraha madogo kufuatia ajali iliyoukumba msafara wa Rais Robert Mugabe alipokuwa akitoka uwanja wa ndege wa Harare.
Katika ajali hiyo ya barabarani, Rais Mugabe mwenyewe hakuumia popote.
Familia hiyo ilikuwa ikitoka nje ya uwanja huo wa ndege walipokuwa wamerejea kutoka Singapore ambapo Rais Mugabe alikuwa akipatiwa matibabu, vilieleza vyombo vya nchini humo.
Shirika la Utangazaji la Zimbabwe lilisema kuwa, Rais Mugabe alifanyiwa upasuaji wa jicho katika nchi hiyo miaka ya nyuma, hivyo alikwenda kwa ajili ya kuangaliwa maendeleo yake.
Msemaji wa Rais aliambia chombo cha habari cha serikali kwamba mke wa rais alilalamikia uchungu katika mkono wake lakini hakuelezea kiini cha ajali hiyo.
Rais Mugabe amekuwa madarakani tangu mwaka 1980 nchi hiyo ilipopata uhuru na amepitishwa na chama chake kuwa mgombea katika uchaguzi mkuu ujao licha ya kuwa na utata juu ya afya ya kiongozi huyo mwenye miaka 93.

from Blogger http://ift.tt/2tti9sP
via IFTTT