MAAJABU: MAMBA AMRUDISHA KIJANA ALIEPOTEA SIKU MOJA (+Video)

Kama binadamu akimuua Mamba mtoni huenda habari hiyo isiwashangaze sana watu ila vipi kama binadamu kakamatwa na mamba halafu baada ya siku moja Mamba huyo akamrudisha mtu huyo? hapo ndiyo habari nyingine ya kustaajabu.
Mwili wa Syarifuddin (41) baada ya kurudishwa na Mamba
Mkazi mmoja wa mji wa Berau nchini Indonesia ajulikanae kwa jina la Syarifuddin mwili wake umerudishwa na Mamba siku moja baada ya kunaswa na Mamba hao alivyokuwa akioga na wenzake mtoni.
Mashuhuda wa tukio hilo ambao alikuwa akioga nao wamesema, Syarifuddin (41) alikuwa akioga kando kando mwa mto Sungai Lempake na ghafla wakataharuki mwenzao akipiga makelele huku Mamba wengi wakimshambulia.
“Alikuwa akioga kando kando ya mto mara ghafla tukaonaakivutwa na Mamba wengi huku akipiga makelele tulishindwa jinsi ya kumuokoa na kwenda kutoa taarifa upesi nyumbani kwao,”amesema Andi Resmin rafiki wa marehemu kwenye mahojiano yake na mtandao wa Malaysian Digest.
Baada ya tukio hilo mashuhuda walienda kutoa taarifa kwa ndugu wa Syarifuddin na ndipo walipoanza mchakato wa kutafuta mwili wake mtoni kwa masaa sita bila mafanikio kabla ya kwenda kutoa taarifa polisi.
Polisi nao walitumia masaa manne kutafuta mwili huo lakini jitihada zao ziligonga mwamba ingawaje walitumia vifaa vya kisasa kutafuta mwili huo.
Moja ya wakazi wanaoishi karibu na mto huo aliyejitambulisha kwa jina la Eet amesema kuna masharti wakati wa kuoga kwenye mto huo inatakiwa muogaji aoge na nguo na akikiuka basi kudakwa na mamba ni rahisi mno.
Hata hivyo baada ya jitihada hizo kukwama ndipo ndugu na jamaa pamoja na wakazi wa eneo hilo walienda kwa Waganga wa Kienyeji na kutambika kwa masaa matatu.
Kwenye matambiko hayo walitumia mijusi mikubwa ambayo inaishi kando kando ya mto huo kwa kuiamrisha kurudisha mwili wa Syarifuddin .
Baada ya Lisaa limoja waliona Mamba mkubwa akitokea mtoni akiwa amebeba mwili wa Syarifuddin akiwa hajajeruhiwa sana lakini tayari akiwa amekufa.
Tazama video ya Mamba akirudisha mwili wa Syarifuddin.n.

from Blogger http://ift.tt/2gMXRcQ
via IFTTT