KIBITI KWAZIDI KUTISHA, MAUAJI MENGINE YATOKEA USIKU WA KUAMIKIA LEO

Wakati Jeshi la Polisi Tanzania likiendelea kuweka mikakati mbalimbali ya kudhibiti mauaji ya raia yanayoendelea Mkoani Pwani, usiku wa kuamkia leo raia mwingine ameuawa na watu wasiofahamika.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Rufiji, Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo ambapo mkazi wa Kitongoji cha Nyambwanda katika Kijiji cha Hanga wilayani Kibiti, Hamis Ndikanye (54) ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Jumamosi akiwa nyumbani kwake.
Kwa mujibu wa maelezo ya ndugu wa marehemu, Hamis Saidi alisema majira ya saa sita za usiku watu takribani watano wakiwa na bunduki walifika nyumbani kwa ndugu yakena kutelekeza mauaji hayo.
Ndugu huyo wa marehemu aliesema kuwa, kabla ya watuhumiwa hao kutekeleza mauaji hayo, walimfunga mke wa marehemu kitambaa usoni na kisha kumpiga risasi mbili mume wake.
Taarifa kutoka kwa Mganga wa Kituo cha Afya Kibiti, Dk Sadock Bandiko zinaeleza kuwa, Ndikaye amepigwa risasi mbili mwilini mwake, moja kichwani na nyingine mgongoni.

from Blogger http://ift.tt/2u9iTIt
via IFTTT