ISHARA ZA MIKONO ZINAZOWEZA KUKUWEKA MATATIZONI KWENYE NCHI NYINGINE

Ishara nyingi za mikono zinazotumika nchini Marekani hutumika sehemu nyingi pia duniani. Ishara hizi bila shaka haziwezi kukusababishia matatizo yoyote, lakini matumizi ya ishara hizo yanaweza kuwa na maana mbaya itayoudhi watu wa tamaduni au nchi tofauti na ya kwako na kukusababishia dhahama ya hali ya juu.
zifuatazo ni baadhi tu ya ishara zinazoweza kuwa salama kuzitumia lakini zikakuweka matatizoni kwenye tamaduni nyingine:
Kisitoria, unapoweka alama ya “V ” kwa vidole vyako unahesabika kumaanisha amani. ‘Alama ya amani’ kwa nchi nyingi ikiwemo Marekani inamaanisha hivyo tu, alama ya amani.
Lakini ukiweka alama hiyo hiyo na kuugeuza mkono wako ukiwa nchini za Uingereza na Australia, utakuwa unamaanisha kitu tofauti kabisa. Kiganja cha mkono kisipotazamana na uso wako ni sawa kabisa kwakuwa hiyo inaweza kumaanisha herufi ‘V’ ikiashiria ushindi ‘Victory’ au ikamaanisha namba mbili. Ni sawa kabisa kuonesha ishara hiyo kiganja chako kikiwa kinaangalia nje, si kwa kukigeuza kwani itakuwa na maana sawa na kumuonesha kidole cha kati huku kwetu.
Alama ya “Pembe za shetani” ni alama ya kawaida kabisa kutumiwa nchini Marekani. Kwa karne nyingi alama hii imekuwa ikitumika nchini humo kumaanisha kitu chenye ubora wa hali ya juu sana au ugumu uliopitiliza. Lakini katika nchi nyingi za ukanda wa Mediterranean kama Italia, alama hii inahusishwa na mapenzi na inabeba maana mbaya kwamba mume/mke wako ana wapenzi wengine zaidi yako.
Alama ya duara inayotokana na kuunganisha ‘kidole cha shahada’ na kidole gumba inamaanisa “sawa, safi, nzuri, hivyohivyo, umepatia” kwa nchi zinazozungumza lugha ya Kiingereza. Lakini kwa nchi za Kusini mwa Amerika kama Brazili inatumika kumtusi mwengine. Rais Mstaafu wa Marekani, Richard Nixon aliwahi kuzomewa nchini Brazili alipoonesha ishara hii mbele ya kadamnasi. Nchini Ufaransa na Ubelgiji pia hutumika kufaninisha uwezo mdogo wa mtu, yaani sifuri, asiye na thamani yoyote.
Kufunga vidole vyako kama ishara ya kuomba ufanikiwe ni ishara inayotumika kwenye nchi nyingi sana kwa maana hiyo lakini usikunje vidole vyako namna hii ukiwa nchini Vietnam. Alama hii nchini Vietnam ina maana sawa na kumuonesha mtu kidole cha kati hapa Tanzania, ni kumtukana.
Ishara ya kulielekeza dole gumba juu au chini ni za kawaida kabisa kumaanisha unakubalia kukataa jambo lililofanywa au kusemwa na mtu. Kwahiyo mara nyingi humaanisha ‘safi, nzuri’ au ‘ndiyo’. Lakini kuinua dole gumba nchini Iran, Afghanistan, Ugiriki na Naijeria – ishara hii ina maana sawa na kumuonesha mtu kidole cha kati hapa Tanzania.
C

from Blogger http://ift.tt/2vquaAq
via IFTTT