“HARMORAPA AKITAKA KUNIOA NIPO TAYARI” SASHA

Mrembo anaetokea sana kwenye vid­eo za Kibongo, Sasha Kas­sim, amevunja ukimya na kudai kwamba, yupo tayari kuolewa na msanii wa Bongo Fleva, Athuman Omary ‘Harmorapa’ kama ataamua.
Akizungumza na 3-Tamu, Sasha alifunguka ya moyoni kuwa, yupo tayari kuolewa na Harmorapa ambaye hivi kar­ibuni alidaiwa kuwa ana uhusiano naye wa kimapenzi.
“Nipo tayari kuolewa na Harmorapa kama akiridhia, sioni ajabu yoyote kwa sababu ni mwanaume rijali kama walivyo wanaume wengine,” alisema Sasha.

from Blogger http://ift.tt/2v0An9H
via IFTTT