Mrembo anaetokea sana kwenye video za Kibongo, Sasha Kassim, amevunja ukimya na kudai kwamba, yupo tayari kuolewa na msanii wa Bongo Fleva, Athuman Omary ‘Harmorapa’ kama ataamua.
Akizungumza na 3-Tamu, Sasha alifunguka ya moyoni kuwa, yupo tayari kuolewa na Harmorapa ambaye hivi karibuni alidaiwa kuwa ana uhusiano naye wa kimapenzi.
“Nipo tayari kuolewa na Harmorapa kama akiridhia, sioni ajabu yoyote kwa sababu ni mwanaume rijali kama walivyo wanaume wengine,” alisema Sasha.
Wabunge wa chama tawala wameunga mkono ripoti ya Taasisi ya Twaweza inayoeleza kushuka kwa ushawishi wa Rais John Magufuli.
Ripoti hiyo iliyotolewa jana na kubainisha kwamba umaarufu wa Rais huyo wa awamu ya tano umeshuka na kwamba anakubalika miongoni mwa maskini, wasio na elimu kubwa pamoja na waishio vijijini.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Lucy Mayenga amesema kilichoelezwa na Twaweza ni sahihi kwa sababu Rais amejielekeza kwa makundi hayo ambayo hayana mtetezi.
“Hao ndiyo watu wengi zaidi. Kiuchumi inakubalika,” amesema Lucy.
Wakati Lucy akiendelea kutoa hoja zake, Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega alitoa taarifa iliyopokelewa na mtoa hoja.
Uledi amesema: “Kwa muda wa utafiti, Rais alikuwa anapambana na vyeti feki, dawa za kulevya na mafisadi. Hao wote hawawezi kumpenda zaidi ya maskini ambao hawaguswi na mambo hayo.”
Lucy ametoa maoni hayo wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Serikali unaoendelea bungeni.
INGAWA Cristiano Ronaldo yuko katika mahusiano ya kimapenzi na kipusa Georgina Rodriguez, ambaye ni mzawa wa Uhispania, nyota huyo wa Real Madrid anatarajia kuwa baba wa watoto pacha wa kiume watakaozaliwa hivi karibuni na mwanamke mmoja mzawa wa Marekani aliyejitolea kuubeba ujauzito huo.
Gazeti la The Sun limesema Ronaldo, 32 aliwahi kutoa mbegu zake za kiume ambazo zilikutanishwa na yai la kichuna mmoja mzawa wa Uhispania aliyelipwa Sh2.8 bilioni kisha mwanamke mmoja mwenye asili ya Amerika akajitolea kuibeba mimba hiyo mwishoni mwa Septemba 2016 kwa kima cha Sh1.5 bilioni.
“Ronaldo ana hamu kubwa ya kuwaona watoto hao ambao watapata hifadhi mpya hivi karibuni katika kasri moja la sogora huyo lenye thamani ya Sh850 milioni jijini Madrid,” ilisema sehemu ya taarifa ya The Sun.
Dolores ambaye ni mama yake Ronaldo, amejitolea kuwalea wajukuu hao kwa kushirikiana na Georgina ambaye kwa sasa anajivunia uhusiano bora zaidi na Ronaldo Jr ambaye ni mwanambee wa sogora huyo,” ilisema habari kwenye magazeti ya udaku nchini Uhispania huku yakisisitiza kuwa jitihada za kumshawishi Ronaldo kutaja jina la mama wa pacha anaowatarajia zimegonga mwamba.
Mapema mwezi jana, Georgina, 23 alimtaka Ronaldo kufanya hima na kurasimisha uhusiano wao wa kimapenzi ndipo amruhusu kabisa kufurahia joto la mwili wake.
Katika mojawapo ya ziara zao za mara kwa mara za kutalii ufuo wa Ibiza nchini Uhispania, kula ujana na kuponda raha, Georgina alimtajia Ronaldo kuhusu kiu aliyonayo ya kumzalia mtoto atakayedhihirisha ukomavu wa penzi alilonalo kwa sogora huyo mzawa wa Ureno.
KAMA ULIMIS VIDEO YA MCHEZAJI WA Ghana ALIE JIKANYAGA KWA KUWASHUKURU MUKE NA MCHEPUKO WAKE TAZAMA HAPA