VIDEO: QUICK ROCKA ADAIWA MILIONI 20 KWA KUIBA WIMBO

Mwanamuziki Khalid Mohamed maarufu kwa jina la sanaa T.I.D amewataka wasanii wenzake wawili kumlipa faini ya Tsh milioni 20 kwa kile alichosema kuwa wametumia haki zake pasipokuwa na idhini yake.
T.I.D amewatakata Quick Rocka na OMG kumlipa fedha hizo baada ya kutumia wimbo wake Watasema Sana bila ridhaa yake jambo ambalo ni kinyume na sheria.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, T.I.D ameweka sehemu ya video ya wimbo huo na kuandika, “Wat is this….?! Hivi ndio mnapata Magari yenu!? @quickrocka & @omgtanzania we need to TALK #Watasema.”
Msanii huyo amesema kuwa wamenakili wimbo wake huo ambao ulimpatia tuzo mbili kutoka nchini Kenya mwaka 2005 (Kisima Music Awards 2005) na hivyo kabla hajafanya kitu kibaya wamlipe fedha hizo.
“Naomba tukutane Central Police huwezi kutumia Haki zangu hivihivi Kabla sijafanya kitu kibaya nahitaji million 20 compensation… This song ni Awards mbili Za Kisima Music Awards 2005 inKenya u can’t just Steal it, Unalala Ndani Leo.”
Video ya wimbo huwa wa Quick Rocka na OMG umetoka leo na unaweza kutazama video hiyo hapa chini;
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2t9qmqv
via IFTTT