Thibaut Courtois akataa kusaini mkataba mpya,Madrid wachekelea.

Mazungumzo ya mwanzo kati ya golikipa wa Chelsea Thibaut Courtois na klabu hiyo yamekwama. Taarifa zinasema klabu ya Chelsea ilikuwa na mazungumzo ya mwazo kuhusu mkataba wa golikipa huyo.
Hata hivyo pande zote mbili zinazozungumza zimeshindwa kufikia muafaka na suala kubwa likiwa ni nyongeza ya pesa katika mkataba huo, lakini wakala wa Courtois atakutana tena na Chelsea kufanya mazungumzo mengine ya pili.
Matajiri wa Real Madrid wanafuatilia kwa karibu suala la mkataba wa Courtois na Chelsea ambaye kwa muda sasa wamekuwa wakitaka kumsajili na kama mazungumzo kati ya Chelsea na Courtois yatashindikana baasi inaweza kuwa njema kwao.
Courtois amekataa mazungumzo ya awali kipindi ambacho golikipa wa Ac Millan Gianluigi Donnaruma amekataa kusaini mkataba mpya na anaweza kuchukua nafasi ya Courtois au anaweza kwenda Real Madrid kama Courtois akisaini mkataba mpya.
 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rCE4wJ
via IFTTT