SIRI YA KIGOGO ALIYESTAAFISHWA NA JPM KUKAA MADARAKANI MUDA MREFU

Siku chache baada Rais Magufuli kumtaka Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji Dar es Salaam (DAWASA), Archard Mutalemwa astaafu, imefahamika kuwa mkataba wake ulikuwa umalizike Oktoba mwaka huu.
Jumatano wiki hii Rais Dkt Magufuli alimuagiza Mutalemwa kustaafu kutokana na kuwa madarakani kwa muda mrefu tangu yeye akiwa shule ya sekondari amekuwa akimsikia kiongozi huyo.
Mtu wa karibu na kiongozi huyo amesema kuwa alistaafu mwaka 2012 na tangu hapo amekuwa akifanya kazi kwa mkataba ambapo mkataba wake wa miaka miwili aloongezewa mwaka 2015 na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete ulikuwa umelizike Oktoba mwaka huu. Alieleza zaidi, Mutalemwa alisema kuwa mkataba wake ukimalizika asingetaka kuongeza tena, na kwamba angeachia nafasi hiyo.
“Alitimiza miaka 60 mwaka 2012, na alitakiwa kustaafu mwaka huo, lakini alipata mkataba wa kuendelea kusalia madarakani kwa miaka mitano ukiwa na kifungu cha kuongeza muda,” kilisema chanzo hicho cha habari ambacho hakikutaka jina lake liweke wazi kwani hakuwa amepewa mamlaka ya kuzungumzia tukio hilo.
Agizo la Rais Dkt Magufuli la kumtaka Mutalemwa kistaafu limemkuta wakati akimalizia muda wa miezi michache iliyosalia kabla ya kuondoka.
Rais alitoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara eneo la Mlandizi Mkoa wa Pwani alipokuwa akifungua mradi mkubwa wa maji wa Ruvu Juu.
Mutalemwa alitakiwa kustaafu ili kulinda heshima yake ambapo Rais Magufuli alimwamba, kuendelea kukaa madarakani zaidi kutapelekea watu kumtafutia jambo la kumchafua. Wakati mwingine sura yako inaweza isizeeke, ila umri ukawa umeenda, hivyo ni vizuri kustaafu kwani ukikaa mahali sana watu watakuzoea, alisema Rais Magufuli.
DAWASA ilituhumiwa na kiongozi huyo wa nchi kuwa, licha ya kupewa fedha za kutosha kusambaza maji Dar es Salaam, Kibaha na Bagamoyo, lakini zimekuwa zikitumika vibaya kutokana na uongozi mbovu.
Chanzo: The Citizen
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2t5lem6
via IFTTT