Simba wanaendelea kuibomoa Azam, safari hii ni Shomari Kapombe

Wakati Azam ikiendelea kunyakua wachezaji kutoka Kanda ya Ziwa, Simba imeendelea kuibomoa Azam na hiyo ni baada ya kufanikiwa kumrejesha mlizi wao wa zamani Shomari Kapombe.
Kapombe amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba lakini bado haijajulikana ni kwa kiasi gani cha fedha.
Mlinzi huyo wa Taifa Stars anarejea kwa mara nyingine kwenye klabu yake ya zamani ambayo ilimtoa na badae akaenda kucheza soka la kulipwa Ufaransa lakini hakudu na aliporejea akajiunga Azam FC.
Kapombe anafanya idadi ya wachezaji wa Azam waliojiunga na Simba kufikia watatu akiungana na John Bocco ‘Adebayor’ na Aishi Manula.

from Blogger http://ift.tt/2ra5rPc
via IFTTT