Rafael Nadal atwaa ubingwa wa French Open kwa mara ya 10.

Baada ya hapo jana mwanadada Jelena Ostapenka kushinda ubingwa wa French Open kwa upande wa wakina dada, hii leo kulikuwa na fainali nyingine kwa upande wa wanaume ambapo Rafael Nadal alikuwa akikabiliana na Stan Wawrinka.
Katika mchezo huo Nadal ameibuka mshindi na hii ikiwa mara ya 10 kwa Mhispania huyo kutwaa taji hili, Nadal aliibuka kidedea katika ushindi huo kwa seti 6-2,6-3,6-1 dhidi ya Wawrinka mwenye miaka 32.
Hili lilikuwa taji la 15 kubwa kwa Raphael Nadal na matokeo haya yamemfanya kukaa juu ya Pete Sempres kwa kushinda Gram Slam nyingi lakini akiwa wa pili nyuma ya Rodger Federer ambaye alipata Grand Slam ya 18 mwezi January baada ya kumfunga Nadal.
Baada ya nchezo huo Rafael Nadal alisema “nimecheza mashindano mengi lakini ushindi huu wa leo hakika furaha yake haielezeki” huku Wawrinka akimuambia “Nadal wewe ni bora sana na mfano bora sana na ninajivunia sana kucheza dhidi yako”
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tc1qdT
via IFTTT