AHUKUMIWA JELA MIAKA 30 KWA KUKIUKA AGIZO LA RAIS MAGUFULI

Mahakama ya Wilaya ya Mlele imemuhukumu mlinzi wa Shule ya Sekondari Ilela kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto wa umri wa miaka 16.
George Sikoki alihukumiwa adhabu hiyo mwishoni mwa wiki na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Teotimus Swai baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.
Mwendesha mashtaka, Baraka Hongoli aliiambia mahakama hiyo kuwa, mshtakiwa George Sikoki alitenda kosa hilo Januari 27 saa 7:30 usiku baada ya kupata taarifa kuwa wazazi wa mtoto huyo wamesafiri na hivyo amebaki peke yake.
Upande wa mashtaka ilesema kuwa, mshtakiwa ambaye ni mlinzi wa shule hiyo iliyopotarafa ya Iyonga wilayani humo alikwenda nyumbani kwa mtoto huyo na kuvunja mlango kisha kumtishia kumuua iwapo angepiga kelele hivyo kumbaka na kutokomea kusikojulikana.
Mwathirika huyo akiwa na maumivu huku akitokwa damu sehemu za siri ilielezwa mahakamani kuwa alijikongoja hadi kwa jirani na kutoa taarifa ndipo alipopelekwa hospitali kwa matibabu.
Mwendesha mashtaka Hongoli alisema, baada ya mshtakiwa kukamatwa alikiri kosa hilo kwa maandishi wakati akihojiwa katika kituo cha polisi, lakini alipofikishwa mahakamani alikana.
Upande wa mashtaka ulipeleka mahakamani mashahidi sita akiwamo daktari aliyethibitisha kubakwa kwa mtoto huyo.
Mahakama hiyo ilisema kuwa, pasipo na shaka wamejiridhisha kuwa mshtakiwa amekutwa na hatia ya kibaka kitendo ambacho ni kinyume na sheria, na hivyo atatumikia kifungo cha miaka 30 jela.
Hukumu hiyo imetolewa ikiwa ni siku chache tangu Rais Magufuli aliposema kuwa, yeyote atakayepatikana na hatia ya kubaka au kumpa mwanafunzi mimba, sheria ipo wazi kuwa ni miaka 30 jela.
Rais Magufuli aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Bagamoyo kuhusu mimba kwa wananfunzi ambapo alisema yeyote atakayepata mimba hatoruhusiwa tena kuendelea na masomo.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tcSOHv
via IFTTT