Mwalimu Nyerere Muda Mfupi Baada ya Uhuru alipata Ugeni wa Siri, Ugeni wa Nelson Mandela. Mandela alikuwa akitaka Msaada kwa Nyerere wa Kuanzisha Jeshi la Kupigania Haki la Umkoto We Skzwe yaani Mkuki wa Bwana au Mkuki wa Mfalme.
Kulingana Na Kitabu cha Mandela cha Long Walk to Freedom, Nyerere alionyesha Kusita, alimshauri asubiri asifanye jitihada za Kijeshi mpaka Walter Sisulu aachiliwe. Wakaagana Nelson akamwambia Mwalimu atarudi Tena na Akaenda Ethiopia ambako alikutana na Haile Selassie, Haile Selassie alimwelewa Mandela Kwa haraka na Akampa Pesa nyingi sana tu. Mandela akasafiri kurudi SA. Kufika huko muda Mchache akakamatwa hivyo hakuweza Tena kuonana na Nyerere.
Baada ya Mandela Kukamatwa na Nyerere Kuona kwa Undani Uonevu wa Ukoloni Nchi za Kusini Mwa Afrika na Ubaguzi wa Rangi SA, basi akaamua Kujitwisha Mzigo wa Kusaidia Majeshi ya nchi zote zile na Pia sio tu hivyo Bali kiwazi wazi akazunguka Dunia Nzima Kupiga Kelele na Pia Kutafuta fedha za kusaidia Majeshi yale. Na mara nyingi akatumia hata Majeshi ya Tanzania kusaidi. Hii ilimhatarisha binafsi na nchi kwa ujumla!
Msumbiji ilipopata Uhuru Nyerere ndiye aliyewakalisha Akina Samora na Kuwaambia wasilipize Visasi kwa Wazungu au Collaborators (Waliokuwa wakiwasaidia wazungu) na kwa Mwongozo wa Moja kwa moja wa Nyerere Ikaanzishwa Tume ya Ukweli na Usuluhishi (Truth and Reconciliation) ambapo waliofanya uhalifu wa kinyama walikuwa wakikiri na Kuomba Msamaha.
South Afrika ilipokuwa Democratic 1994 Mandela Akafuata Mfano huo nukta kwa Nukta. Lakini Dunia Nzima ikamwenzi sana Mandela, Mandela alizikwa na Viongozi wote Wa dunia, Ila Nyerere hakupewa heshima wala shukurani anayoistahili na Dunia wakati wa Kifo chake.
Kila uendapo Duniani Unakuta Sanamu za Mandela, Ila Nyerere hata AU ilibidi Mugabe aseme ikiwa Afrika haitaki Kumkumbuka Nyerere Zimbabwe itafanya Kivyake!
from Blogger http://ift.tt/2qfrELz
via IFTTT