Kwa baadhi ya vitendo au maamuzi yanayofanywa na huyu kiongozi kwa kutumia cheo chake yananifanya niamini kumbe hata mimi naweza kuongoza vizuri na kwa busara kuliko huyu.
Kitendo cha kukamata watu walioenda kufarijiana kwa msiba uliotokea eti ni mkusanyiko usio halali eti hauna kibali, hata atumie hoja nyingi kias gani kujisafisha ukweli utabaki palepale
Ameivua nguo serikali na mamlaka iliyomteua.
Kitendo hiki kimepanda chuki juu yake kwa sababu kuna watu wengi wapo nyuma ya waliokamatwa mfano wale viongozi wa dini. Yaani hapo wisdom empty hata kama itatumika jiki kusafisha hilo halitoki kwenye mioyo ya watanzania.
Hata kama nitakamatwa mimi mtoa hoja, bado ukweli utabaki hapo na cheo chako ni dhamana tu kesho tutakuwa wote huku mtaani. Sidhani kama alifikiri vizuri impact ya kitendo hiki, bado najiuliza hivi asingewakamata na kuwalaza polisi kwani kuna madhara yangetokea?
Jambo la pili ni kuhusu rambi rambi..
Najiuliza; Je, kama serikali inatumia rambirambi kinyume na matakwa ya waliotoa rambirambi na yenyewe ipo tayari fedha inazotuma kwenye halmashauri nchini zitumike kinyume na maelekezo?
Nakumbuka mara kadhaa waziri mkuu amekuwa akitoa onyo kali kwa viongozi kunapokuwa na fungu fulani limetolewa kwa shughuli fulani kwamba zitumike kama ilivyopangwa.
Chanzo – JF
from Blogger http://ift.tt/2qfdzxG
via IFTTT