TzTown Tv: SOKO LA KAHAWA NJOMBE LAPATIKANA BRAZIL

WAKAZI mkoani Njombe wamedaiwa kuvuna miti michanga kutokana na kuto kuwa na mazao ya kibiashara ambayo yanaweza kuendesha maisha wakati wakisubiri miti yao kukomaa kitu kinacho sababisha kuingiza mbao mbovu sokoni na kuikosesha serikali Fedha za kutosha kutokana na mapato yatokanayo na miti.
Inaelezwa kuwa kuto kuwapo kwa mazao ya kuvunwa kila mwaka kama Miparachichi na Kahawa ndio chanzo cgha uvunaji wa Miti ambayo haijafikia muda wa kuvunwa.
Halamashauri ya wilaya ya Njombe baada ya kubaini kuwa kuna hali ya kuwapo kwa uvunaji wa miti ambayo haija komaa na kusababisha mapato kidogo kutokan ana eneo lililovunwa Mwenye Halamashauri hiyo anawataka Madiwani katika Baraza lake kwenda kuwahamasisha wananchi kupanda miti ya Matumba.
Je nini kiliondoa Kahawa inayo hamasishwa kulimwa katika mashamba ya wakazi wa mkoa wa Njombe hapa inaelezwa huku Brazil ikidaiwa kuwa ni soko.
Kwa miaka mingi mkoa wa Njombe ukekuwa ukipanda miti kwaajili ya mbao ambayo ili kuvunwa ni lazima ishikilie ardhi bila kuzalisha kitu kingine kwa miaka zaidi ya kumi huku ukiisubiri kupata mavuno lakini miti ya matunda inayo hamasishwa ni miaka mitatu pekee unaanza kuingiza pesa na hapo ni kila mwaka tofauti na miti ya mbao ambayo sasa huvunwa kabla ya mda wake.

TAZAMA VIDEO SOKO LA KAHAWA NJOMBE LAPATIKANA BRAZIL……………….


from Blogger http://ift.tt/2sboE3R
via IFTTT