Mangu Amsukumia Sakata la Mauaji Mkoani Pwani IGP Sirro..!!!

Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu amewataka wananchi kumpa ushirikiano IGP mpya, Simon Sirro katika kukabiliana na matukio ya uhalifu nchini hasa katika Mkoa wa Pwani.
Mangu ameyasema hayo leo Ikulu jijini Dar es salaam baada ya Rais John Magufuli kumwapisha Sirro kuwa IGP mpya wa kuliongoza jeshi la polisi nchini.
Kuhusiana na hali inayoendelea mkoani Pwani, Mangu amesema “Sirro anafahamu anachotakiwa kufanya katika hilo, nimefanya naye kazi kwa karibu, ninachoomba ni askari na wananchi wote wampe ushirikiano” – Mangu alifunguka
Mangu ambaye anasubiri kupangiwa kazi nyingine amesema anamfahamu Sirro kama mchapakazi mzuri na ataweza kutekeleza majukumu yake ya kuhakikisha kwamba Tanzania inakuwa na amani

from Blogger http://ift.tt/2qBPL6l
via IFTTT