Rungwe Amkalia Kooni Paul Makonda Sakata la vyeti Siasa

Rais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe Spunda amemshauri Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kujitokeza hadharani na kutoa ufafanuzi juu ya utata wa jina lake unaozidi kuvuma mitandaoni
*
Utata huo unadaiwa kutokana na mkuu huyo wa mkoa kutumia cheti cha mtu mwingine cha kidato cha nne kujiendeleza kielimu. 
Rungwe ametoa ushauri huo leo kupitia kipindi cha maswali na majibu cha Kikaangoni , akimsisitiza Makonda kuweka ukweli mezani na kuacha kupiga chenga za mchangani kwa maana akiendelea kukaa kimya watu wanazidi kuamini uvumi huo. “Namshauri Mkuu wa mkoa ambaye ni kama mwanangu, atoke azungumze ili kumaliza huu utata wa vyeti, asimsumbue Rais ana mambo mengi” Amesema Rungwe
*
Pia, amemtaka kuacha kulia madhabahuni, kwakuwa hilo halitamsaidia kwa kuwa kulia siyo jibu, na atambue kuwa ofisi hiyo aliyopo sasa siyo yake bali ni wananchi, hivyo kila alichokikuta atakiacha. “Siku moja nafungua ‘ipad’ yangu namuona Mkuu wa Mkoa analia mbele ya kanisa halafu mchungaji anambembeleza kama mjukuu wangu, mimi namwambia kulia kwake hakusaidii kitu yeye anapaswa kusema ukweli tu kama hilo jina siyo la lake halisi ila ni la kisanii sisi tutamuelewa”. Alisema Rungwe
*
Aidha Rungwe aliendelea kufunguka kwa kumtaka Makonda kuacha kung’ang’ania nafasi ambazo anastahili katika nafasi hiyo huku akimpiga kijembe kuwa mwanaume hachagui kazi aende akabebe hata zege kama hana ujuzi wa kufanya.
*
Alimaliza Hivyo Ndugu Rungwe.. Nini maoni yako mdau.. Unamuunga mkono Rungwe au unapingana naye???


DOWNLOAD APPS YA TZTOWN HAPA

http://ift.tt/2ms2574
WANANCHI WAOMBA SERIKALI KUODOA TAKA KIZIMBANI MAKAMBAKO MKOANI NJOMBE


from Blogger http://ift.tt/2nqjmTc
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2nqxtb2
via IFTTT

from Blogger http://ift.tt/2mx7VFd
via IFTTT




from WordPress http://ift.tt/2mvYxkp
via IFTTT